Most Popular

MATUKIO DUNIANI

 

15.09.2016

Lula atuhumiwa kuwa "kiongozi mkuu" wa mtandao wa rushwa

Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva na mkewe Marisa Leticia Agosti 15, 2016 katika mji wa Sao Paulo
 Nchini Brazil, mwendesha mashitaka anayehusika na uchunguzi wa kashfa ya rushwa katika kampuni ya umma ya mafuta ya Petrobras, aliomba Jumatano, Septemba 14 kushtakiwa kwa rais wa zamani Lula kwa rushwa na kujitajirisha kinyume cha sheria.ENDELEA

 

 

15.09.2016

Jenerali Khalifa Haftar apokelewa Ndjamena na Rais Déby

 Jumanne wiki hii jenerali muasi alijielekeza katika mji mkuu wa Chad, Ndjamena. Alipokelewa na Rais Deby, ambaye alikuwa alimuomba kukutana naye.ENDELEA

 

14.09.2016

Babu auzaye aiskrimu ateka nyoyo za wengi 

 Fidencio Sanchez, 89, alilazimika kustaafu majira ya kiangazi, baada ya bintiye kuaga dunia, na ikambidi awe mlezi wa wajukuu wake.ENDELEA

 

 

14.09.2016

Nicolas Sarkozy na David Cameron waliongoza kampeni dhidi ya Gaddafi

 

 

14.09.2016

Marekani kupeleka misaada ya kijeshi Israel kwa mkataba wa dola Bilioni 38

 

Katika mkataba huo Israel watapokea dola milioni 500 kwa mwaka kwa ajili ya mpango wa ulinzi wa makombora.ENDELEA

 

12.09.2016

Mapigano yazuka kumiliki visima vya mafuta nchini Libya 

 Afisa mmoja wa usalama amekanusha kuwa vikosi vinavyomtii jenerali Khalifa Haftar vinadhibiti miji ya Sirda, Ras Lanuf na ZuitinaENDELEA

 

 

12.09.2016

Waasi waonyesha wasiwasi kusitishwa mapigano nchini Syria 

Miundombinu na majengo vimeharibiwa vibaya
Kuna madai kuwa moja ya kundi la waasi la Ahrar al-Sham watakataa kusitisha mapigano hayo.  ENDELEA

 

  12.09.2016

Shambulio la kigaidi latibuliwa Mombasa

Kituo cha police cha Central mjini Mombasa Kenya
  Maafisa wa polisi nchini Mombasa wanasema kuwa walitibua jaribio hilo na kufanikiwa kuwaua wanawake watatu huku wawili wakikamatwa.ENDELEA

 

12.09.2016

Mo Farah afedheheshwa katika uwanja wa ndege Marekani 

 

Farah ambaye alihifadhi taji lake katika mbio za mita 5,000 na 10,000 katika michezo ya Olimpiki ya Rio pamoja na familia yake walikuwa wakisafiri kutoka Atlanta kuelekea nyumbani kwake huko Partland Oregon.

 

 12.09.2016

Hilary Clinton augua homa ya mapafu

 

 Clinton aliondoka mapema, picha zilizowekwa mtandaoni zinamuonesha akisaidiwa na msaidizi wake, huku akitaka kuanguka alipokaribia kwenye gari, lakini baadae bi clinton alitokea kwenye nyumba ya mwanae na kuwaambia waandishi wa habari kuwa anajisikia vizuriENDELEA

10.09.2016

Ugiriki katika hatari ya kutopata mkopo zaidi 

 Mawaziri wa fedha wa mataifa wanachama wa umoja wa ulaya wanajiandaa kukutana ugiriki,Taifa hilo limeonyesha dalili huenda likashindwa kufikia ahadi za kiuchumi ilizotakiwa, kupata sehemu nyingine ya mkopo inaohitaji.ENDELEA

 

10.09.2016

Polisi Ufaransa inawahoji wanawake 3 kwa tuhuma za ugaidi 

Mmoja wa raia aliowaona wanawake hao kabla ya kukamatwa kwenye eneo la Boussy-Saint-Antoine, kusini mwa jiji la Paris, amesema wanawake hao walikuwa na hofu muda mwingi na walikuwa wakitazamatazama pande walizokuwa wakitokea.ENDELEA

 

 

10.09.2016

Amani Syria: Marekani na Urusi zaafikiana  

 
Matokeo ya vita vya kiraia nchini Syria

  Marekani na Urusi zimekubaliana mpango unaolenga kumaliza vita nchini Syria na kuanza mchakato wa mpito wa kisiasa.ENDELEA

10.09.2016

Maji ya mto yageuka 'rangi ya damu' Urusi 

 

Wachunguzi wa masuala ya mazingira nchini Urusi wanajaribu kubaini sababu iliyoyafanya maji ya mto ulio karibu na kiwanda cha nikeli cha kampuni ya Norilsk Nickel kubadilika na kuwa ya rangi nyekundu.ENDELEA

10.09.2016

  Korea Kaskazini yalipua bomu la nyuklia sawa na la Hiroshima

Bomu lililoangushwa Hiroshima mwaka 1945 lilikuwa na nguvu ya kilo tani 15 (tani 15,000).
Bomu lenye nguvu zaidi la nyuklia lililowahi kulipuliwa lilikuwa lile lililopewa jina Tsar-bomba, ambalo lililipuliwa na Urusi mwaka 1961.ENDELEA

 

O9.09.2016

 Uratibu wa mashirika ya kiraia katika mkoa wa Tanganyika ulitangaza Alhamisi hii Septemba 8 kuwa "shughuli zitasimama" katika mji wa Kalemie kwa kupinga dhidi ya kukithiri kwa ukosefu wa usalama katika mji huo.ENDELEA

 

O9.09.2016

Obama akutana na rais wa Ufilipino aliyemtusi 

 Mzozo Kati ya Obama na Dulerte ulianza wakati Obama alibaini kwamba angemuuliza kiongozi Rais Rodrigo Dulerte maswali kuhusiana na mauaji ya kiholela ya watu wanaotuhumiwa kuhusika katika ulanguzi wa madawa ya kulevya nvchini Ufilipino.ENDELEA

 

O9.09.2016 

Walimu zaidi ya 10,000 wasimamishwa kazi Uturuki

Recep Tayyip Erdogan, katika mji wa Ankara Julai 29, 2016 aendelea na operesheni yake ya kuwasimamisha kazi wafanyakazi mbalimbali wa umma. .
 Alhamisi wiki hii Serikali ya Uturuki imewasimamisha kazi walimu zaidi ya 10,000 wakituhumia kuwa na uhusiano na kundi la wapiganaji la PKK katika hali ya kamata kamata katika sekta ya elimu baada ya mapinduzi yaliyoshindwa ya Julai, afisa mmoja wa Uturuki ametangaza.ENDELEA

 

O9.09.2016 

Wezi wazima safari ya bajaji ya kawi ya jua Ufaransa

 
Aiwa nje ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Alexander Nevski mjini Sofia, Bulgaria

 Safari ya miezi saba ya bajaji inayotumia kawi ya jua na nguvu za umeme, ambayo ilikuwa inatoka India kwenda hadi Uingereza, imesitishwa kwa muda baada ya wezi kuiba hati ya kusafiria ya dereva wa gari hilo karibu na mji wa Paris.ENDELEA

O9.09.2016 

Mwanamke avunja rekodi ya ndevu ya Guinness World Record

 Mwanamitindo mwenye ndevu za urefu wa inchi sita ametambuliwa na Guinness World Record kuwa mwanamke wa umri mdogo zaidi duniani kuwa ndevu zilizokomaa kabisa.ENDELEA

O7.09.2016

 Mhubiri wa kiislamu Choudary ahukumiwa kifungo cha miaka mitano jela 

 

  Mhubiri wa Kiislamu mwenye msimamo mkali wa kidini Anjem Choudary, alihukumiwa Jumanne miaka mitano na nusu gerezani na mahakama ya London kwa kosa la kutoa wito wa kuunga mkono wanajihadi wa kundi la Islamic State (IS).ENDELEA

 

O7.09.2016 

Askari watatu wa Uturuki wameuawa Jumanne hii kaskazini mwa Syria katika shambulizi la kwanza baya kabisa kuhusishwa kundi la Islamic State (IS) tangu kuanza kwa mashambulizi ya Uturuki wiki mbili zilizopita, kwa mujibu wa vyanzo rasmi.ENDELEA

07.09.2016

 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshutumu vikali hatua ya Korea Kaskazini kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu siku ya Jumatatu.ENDELEA

 

07.09.2016

Mfahamu rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte, kiongozi aliyemtusi Obama 

 Rodrigo "Digong" Duterte ni kiongozi ambaye msimamo wake na matamshi yake huzua utata mara kwa mara. Amegonga vichwa vya habari tena baada ya kuonekana kumtusi Rais wa Marekani Barack Obama na kumuita "mwana wa kahaba".ENDELEA

 

07.09.2016

Mahakama moja nchini Ufaransa iliyoko pwani ya mji wa Corsica, imesita kutoa amri ya katazo kwa wanawake wavaa vazi la burkini,vazi hilo ambalo mwanamke avaapo huanzia kichwani na kustiri mwili wote, na hupendwa mno na wanawake wa Kiislam.ENDELEA

 

07.09.2016

Aliyefanyiwa upandikizaji wa kwanza wa uso afariki 

 Madaktari nchini Ufaransa wamefichua kwamba mwanamke aliyefanyiwa upasuaji wa kwanza wa upandikizaji wa sura alifariki mapema mwaka huu.ENDELEA

 

 

 

05.09.2016

Korea Kaskazini yarusha makombora mkutano wa G20 ukiendelea China

 
ENDELEA

 

05.09.2016

Ethiopia:Watu kadhaa wauawa katika gereza la Qilinto

Habari ambazo hazijathibitishwa na serikali ya Ethiopia zinasema kwamba sisasi nyingi zilifyatuliwa Jumamosi Agosti 3 katika gereza lenye ulinzi mkali, lililo karibu na mji mkuu, Addis Ababa. Inaarifia pia kuwa moto uliwashwa katika gereza hilo.ENDELEA

 05.09.2016

IS yapoteza ngome zake zote kwenye mpaka wa Uturuki na Syria

 

Waziri Mkuu wa Uturuki Binali Yildirim, alisema Jumapili hii Septemba 4 kwamba mpaka wa Uturuki na Syria sasa uko salama kabisa na vikosi vya Uturuki vinadhibiti eneo hilo. Kundi la Islamic State limepoteza maeneo iliyokua ikiyashikilia hivi karibuni.ENDELEA

 

05.09.2016

Marekani na Urusi bado sana kufikia makubaliano kuhusu mzozo wa Syria

 Serikali ya Marekani imesema mpaka sasa hawajafikia hatua yoyote ya kukubaliana na nchi ya Urusi kuhusu kumaliza vita nchini Syria, ikiutuhumu utawala wa Moscow kwa kurejesha masuala ambayo ilidhani walishayamaliza.ENDELEA

 

 05.09.2016

Kanisa katoliki lamtangaza Mother Teresa kuwa mtakatifu

 

Sherehe za kumtangaza Mama Teresa kuwa mtakatifu zilifanyika kwenye ibada maalumu ya utakaso kwenye uwanja wa St Peters, ikiongozwa na Papa Francis mbele ya waumini zaidi ya laki moja waliohudhuria.ENDELEA

 04.09.2016

Macho yatolewa katika kisa cha ''ushirikina Nigeria

 

 Kijana mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa jimbo la kaskazin magharibi mwa Nigeria la Bauchi anasema kuwa macho yake yalitolewa na watu waliotaka kuyatumia kwa ajili ya sababu za ushirikina.ENDELEA

04.09.2016

Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby amekubali kwamba alikuwa na habari kwamba askofu Nicholas Chamberlain ni baladhuli na shoga na kwamba alimteua kuwa askofu kutokana na umahii wake.ENDELEA

 

04.09.2016

Bikizee wa miaka 87 afungwa karibu mwaka mzima jela Ujerumani, kisa...

 Bikizee mmoja wa miaka 87 amehukumiwa kifungo cha miezi minane jela na mahakama moja ya nchini Ujerumaini kwa kosa la kukanusha tukio lililojaa utata la kuuliwa kwa umati Mayahudi nchini humo, maarufu kwa jina la ngano ya Holocaust.ENDELEA

 

04.09.2016

Marekani na China zaridhia mkataba wa Paris

 

Rais wa China Xi Jinping na Rais Barack Obama wa Marekani wamewasilisha nyaraka hizo kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon huko Hangzhou, China hii leo. ENDELEA

04.09.2016

Rais Xi Jinping wa China afafanua ufumbuzi wa kichina kwenye ufunguzi wa mkutano wa kilele wa G20

 

Hivi sasa uchumi wa dunia unaendelea kudidimia, huku kasi ya ongezeko la biashara ya kimataifa ikifikia kiwango cha chini zaidi katika miaka 30 iliyopita. Wakati huohuo, changamoto za kisiasa na kiusalama duniani pamoja na masuala mbalimbali ya kikanda, vimetatanisha zaidi uchumi wa dunia. Katika hali hiyo, jumuiya ya kimataifa imekuwa na matarajio makubwa kwa China. Kwenye hotuba yake, rais Xi Jinping wa China ametoa ufumbuzi wa kichina kwa uchumi wa dunia unaokabiliwa na matatizo.ENDELEA

03.09.2016

Watu 500 waripotiwa kupoteza maisha yao kwa ugonjwa wa kipindupindu Kongo DR

 Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, jumla ya watu 500 wamepoteza maisha yao nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kutokana na ugonjwa wa kipindupindu.ENDELEA

 

 

03.09.2016

 

FBI yatoa ripoti ya uchunguzi dhidi ya Hillary Clinton kuhusu kashfa ya nyaraka za siri

Mapema mwaka huu FBI walisema kuwa Hillary alipaswa kuwa mwangalifu zaidi katika kutunza nyaraka za siriENDELEA

 

 03.09.2016

Naibu rais azindua kondomu zenye ladha Afrika Kusini

 Naibu wa rais nchini Afrika Kusini alichukua fursa bungeni wakati ambapo rais wa taifa hilo Jacob Zuma alikuwa amesafiri nje ya nchi kuwakilisha maswala ya serikali ikiwemo kondomu isiyo na kelele na yenye ladha ya machungwa kwa wabunge.ENDELEA

03.09.2016

 

Satelaiti ya Facebook ya kufikisha mtandao kasi Afrika yaharibiwa

Roketi ya Falcon 9 ilipolipuka
 Satelaiti hiyo kwa jina Amos-Six ilikuwa imebebwa na roketi ya Falcon Nine ambayo ililipuka ilipokuwa ikifanyiwa majaribio ya kujiandaa kwa safari ya siku ya Jumamosi.
Mlipuko huo ulitokea wakati roketi hiyo ilikuwa ikijazwa mafuta na kutikiza majengo yaliyokuwa umbali wa kilomita kadhaENDELEA

 03.09.2016

Jackie Chan kupewa tuzo ya Oscar ya staha

 

 Mwelekezi na mwigizaji mashuhuri wa filamu Jackie Chan atapokea tuzo ya staha ya Oscar kwa mchango wake mkubwa katika tasnia ya filamu.ENDELEA

02.09.2016

Melania Trump ashtaki gazeti kuhusu tuhuma za ukahaba

Tuhuma kwamba alifanya kazi kama kahama ni uongo mtupu, wakili wake amesema.

 

Melania Trump amelishtaki gazeti la Daily Mail la Uingereza pamoja na mwanablogu wa Marekani akitaka alipwe $150m (£114m) kuhusiana na tuhuma kwamba alikuwa kahaba miaka ya 1990, wakili wake amesema.ENDELEA

 

02.09.2016

Jua lapatwa Afrika

kupatwa kwa jua

 

Picha nzuri ni zile zilizoonekana nchini Tanzania ambapo tukio hilo lilichukua mda wa dakika tatu.
Kupatwa huko kwa jua pia kulionekana nchini Gabon,Congo-Brazaville,DRC Madagascar na kisiwa cha Re-union.ENDELEA

 

0 2.09.2016

Seneta afananishwa na 'kahaba mwenye hasira' Australia

Seneta Jacqui Lambie

 

Seneta mmoja anayependa kuzungumza sana nchini Australia amemfananisha na ''kahaba mwenye hasira'' mwenzake wa chama cha kihafidhina kabla ya kuomba msamaha kwa makahaba.ENDELEA

02.09.2016

Marcel Lazar, mdukuzi wa watu maarufu adakwa Marekani

 

Mahakama moja nchini Marekani imemfunga jela raia moja mwenye asili ya nchini Romania kwa kosa la udukuzi mtandaoni kwa watu wenye hadhi za juu nchini humo ikiwemo familia ya Bush.ENDELEA

02.09.2016

Mark Zuckerberg ala ugali Kenya

 

 Zuckerberg aliyewasili siku ya Jumatano kutoka nchini Nigeria alifanya kikao na waziri wa habari nchini Kenya Joseph Mucheru,ambapo walizungumza kuhusu mtandao na mipango ya serikali kuhakikisha kila kijiji kimeunganishwa na mtandao.ENDELEA

 

01.09.2016

Walanguzi 2 wa biringanya kutoka Burundi wauawa Rwanda

 Walanguzi wawili wa biringanya raia wa Burundi wameuawa jana usiku upande wa Rwanda wa mpakani, kwa mujibu wa msemaji wa polisi wa Burundi, Pierre Nkurikiye.ENDELEA

01.09.2016 

Waziri aliyesinzia mkutanoni auawa Korea Kaskazini

Serikali ya Korea Kusini imesema waziri wa elimu nchini Korea Kaskazini ameuawa na maafisa wa serikali.ENDELEA

 

 

01.09.2016 

Kokeini yenye thamani ya Euro milioni €50 imepatikana katika kiwanda cha Coca-Cola

Kokeini yenye thamani ya bei ya mtaani kiasi cha Euro 50 m imegundulika katika kiwanda cha a Coca-Cola kilichopo kusini mwa Ufaransa.
Dawa hiyo iliyokuwa imefichwa kwenye mifuko ya kuuzia juisi ya machungwa , ilifika kwenye shehena kutoka Amerika KusiniENDELEA

 

01.09.2016

John Kerry akwama kwenye foleni Delhi, India

Add caption
  Mvua kubwa ilinyesha na 'kukosa kutambua cheo chake'.Badala ya magari yake kupitia barabara zilizo wazi, msafara wake wa magari ulikwama kwenye foleni zaidi ya saa moja.ENDELEA

 

31.08.2016

Wazayuni wakiri wajibu wa kuundwa nchi huru ya Palestina

 Mkuu wa zamani wa Shirika la Kijasusi la Israel MOSSAD amesema, suala la kuundwa nchi huru la Palestina ni jambo lisiloepukika.ENDELEA

 

31.08.2016

Mmoja wa makamanda wa IS auawa nchini Syria

 

 Kundi la wapiganaji la Islamic state limetangaza kuwa mmoja wa kamanda wake mwandamizi ambae ni msemaji wa kundi hilo, Abu Muhammad al-Adnani ameuwawa nchini Syria.ENDELEA

31.08.2016

Mapacha waliozaliwa wameungana wanajiandaa kuanza shule


 Mama yao , Angela Formosa, amesema watoto hao ambao kwa sasa wana umri wa miaka minne , kutoka eneo la la Bexleyheath Kusini mashariki mwa mji wa London ,"wanafuraha sana " ya kuanza shule.ENDELEA

31.08.2016

Mfungwa aapishwa kuwa Meya wa karachi

 

 Mfungwa mmoja ameapishwa kuwa meya mpya wa mji mkuu wa Pakistan-Karachi.ENDELEA

31.08.2016

Sheria tata za mtindo wa nywele katika shule za sekondari A.Kusini zasitishwa

Picha ya mmoja wa waandamanaji
 Sheria kuhusu namna wasichana wa shule za sekondari wanavyochana nywele nchini Afrika Kusini zimesitishwa baada ya maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi yaliyofanywa na wanafunzi weusi, ameleza waziri nchini humoENDELEA

 

31.08.2016

Shambulio la hoteli lawaua watu 12 Somalia

Hoteli ya SYL nchini Somalia
 Hoteli hiyo imeshambuliwa mara kadhaa na al-Shabab katika miaka ya hivi karibuni..ENDELEA

 

 30.08.2016

Mkahawa wakataa kuwahudumia wanawake Waislamu Ufaransa

 Kanda ya video mjini Paris ilioonyesha mkahawa mmoja ukikataa kuwahudumia wanawake wawili Waislamu imezua hisia kali nchini Ufaransa.ENDELEA

30.08.2016

AFRIKA KUSINI:Wanafunzi weusi wapinga amri ya kuwataka walainishe nywele

Wanafunzi wanasema kuwa amri hiyo ni ya kibaguzi

 

 Kumeshuhudiwa maandamano kwenye shule moja ya wasichana nchini Afrika Kusini baada ya wanafunzi weusi kuambiwa na shule moja mjini Pretoria, wazilainishe nywele zao.ENDELEA

 30.08.2016

Maelfu ya wahamiaji waokolewa katika pwani ya Libya

Vikosi vya uokoaji vya majini vya Italy vimesema vimeratibu uokoaji wa wahamiaji elfu sita na mia tano katika bahari ya Mediterania siku ya jumatatu. Kwa mujibu wa vikosi hivyo, hii ni oparesheni kubwa zaidi kuwahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni.ENDELEA

 makao makuu ya polisi yateketezwa uturuki

Bomu kubwa la kutegwa ndani ya gari limelipuka kwenye makao makuu ya polisi wa kutuliza ghasia mjini Cizre, kusini mashariki mwa Uturuki na kuwauwa polisi 11, na wengine 70 wamejeruhiwa 
Haijafahamika ni nani aliyetekeleza shambulio hilo, lakini vyombo vya habari vya Uturuki vimelaumu chama cha wafanyakazi wa kikurdi kilichopigwa marufuku cha -PKK - kuhusika na shambulio hilo.

Wakazi wa mji wa Cizr wamekuwa chini ya tahadhari ya kutotoka nje kwa miezi kadhaa iliyotangazwa na mamlaka za Uturuki zinazopigana dhidi ya PKK.ENDELEA

 26.08.2016

Mzozo wa PKK Uturuki: Shambulio la bomu lawauwa polisi 11

 

Bomu kubwa la kutegwa ndani ya gari limelipuka kwenye makao makuu ya polisi wa kutuliza ghasia mjini Cizre, kusini mashariki mwa Uturuki na kuwauwa polisi 11, na wengine 70 wamejeruhiwa 
Haijafahamika ni nani aliyetekeleza shambulio hilo, lakini vyombo vya habari vya Uturuki vimelaumu chama cha wafanyakazi wa kikurdi kilichopigwa marufuku cha -PKK - kuhusika na shambulio hilo.

Wakazi wa mji wa Cizr wamekuwa chini ya tahadhari ya kutotoka nje kwa miezi kadhaa iliyotangazwa na mamlaka za Uturuki zinazopigana dhidi ya PKK.

26.08.2016

Mwanamume India abeba maiti ya mkewe 12km

Wakati akitembea , Bw Majhi alisindikizwa na mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 12 , Chaula
Mwanamume mmoja maskini nchini India alibebe maiti ya mkewe kwa zaidi ya kilomita 12 baada ya hospitali alimofariki kushindwa kumsafirisha kwa gari la kuwabebea wagonjwa hadi kijiji mwake.

Mke wa Dana Mjhi, Amang, mwenye umri wa 42, alifariki dunia baada ya kuugua maradhi ya kifua kikuu katika hospitali ya Ulaya, mji wa Bhawanipatna jimbo la Orissa. ENDELEA

 

26.08.2016

Waliofariki Italia wafika 247, manusura watafutwa

 Idadi ya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi katikati mwa Italia mapema Jumatano imefika 247 huku manusura wakiendelea kutafutwa.

Maafisa wa uokoaji wanaendelea na juhudi za kutafuta manusura na miili kwenye vifusi.
Manusura eneo la Amatrice wakesha chini ya mti usiku

Tetemeko hilo la nguvu ya 6.2 katika vipimo vya Richter liliharibu vibaya miji ya Amatrice, Accumoli na Pescara del Tronto ambapo watu wengi walifariki.ENDELEA

 24.08.2016

Athari ya Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya

Juni 23 Uingereza ilipiga kura ya kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya EU katika kura ya maoni iliyofanyika nchini humo. Katika uchambuzi wa habari utamsikia Hidetoshi Nakamura Profesa mshiriki wa Chuo Kikuu cha Waseda katika kitivo cha sayansi ya siasa na uchumi, akizungumzia matatizo yanayoweza kujitokeza baada ya Uingereza kujiondoa EU pamoja na vile kujiondoa huko kunaweza kuathiri maeneo mengine.ENDELEA

 

24.08.2016

Jeshi la Nigeria: Makamanda watatu wa Boko Haram wameuawa, kiongozi wao amejeruhiwa vibaya

Kiongozi wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram la nchini Nigeria inaaminika kuwa amejeruhiwa vibaya katika shambulio la anga lililofanywa na jeshi kaskazini mashariki mwa nchi. Hayo ni kwa mujibu wa duru rasmi za jeshi la nchi hiyo.
Abubakar Shekau, kiongozi wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram
 Jeshi la anga la Nigeria limetangaza leo kuwa siku ya Ijumaa, ndege za kivita za jeshi hilo zilifanya shambulio kwenye msitu wa Sambisa. Msemaji wa jeshi, Kanali Sani Kukasheka Usman amesema makamanda watatu wa kundi hilo Abubakar Mubi, Malam Nuhu na Malam Hamman wameuawa; na kiongozi wao anayejulkana kama 'Abubakar Shekau' inaaminika kuwa amejeruhiwa vibaya mabegani.ENDELEA

 

 24.08.2016

Adha ya mafuriko India
Zaidi ya watu 300 wanaripotiwa kufariki dunia nchini India kufuatia janga la mafuriko yaliyotokea mashariki na katikati mwa nchi hiyo.

Duru rasmi za serikali ya India zinaripoti kwamba, mafuriko hayo yameharibu kabisa vijiji, mazao na barabara katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko hayo.ENDELEA

24.08.2016

ITALIA:TETEMEKO LA ARDHI LAUA WATU SITA

Tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 6.2 katika vipimo vya Richter limetikisa eneo la Umbria katikati mwa Italia na kufukua watu chini ya vifusi, maafisa wa Italia wamesema.
Tetemeko hilo lilitokea mwendo wa saa tisa na dakika thelathini na sita usiku saa za Italia (01:36 GMT), 76 km (maili 47) kusini mashariki mwa mji wa Perugia, katika kina cha 10km (maili sita) chini ya ardhi, taasisi ya Marekani inayohusika na mitetemeko ya ardhi USGS imesema.ENDELEA

 

 

 22.08.2016

Mripuko wauwa 50 katika tafrja ya harusi Uturuki

Takriban watu 50 wameuwawa Jumamosi(20.08.2016) wakati anayetuhumiwa kuwa mripuaji wa kujitowa muhanga alipojiripuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakicheza ngoma mtaani wakati wa sherehe ya harusi kusini mwa Uturuki.


Takriban watu 50 wameuwawa hapo Jumamosi(20.08.2016) wakati anayetuhumiwa kuwa mripuaji wa kujitowa muhanga aliporipuwa vilipuzi vyake miongoni mwa watu waliokuwa wakicheza ngoma mtaani wakati wa sherehe ya harusi kusini mwa Uturuki.ENDELEA

 

Afungwa miaka 5 jela kwa kumtesa mbwa Marekani

Mwanamume mmoja nchini Marekani amekiri kosa la kuufunga mdomo wa mbwa mwaka jana America Vyombo vya habari katika jimbo la South Carolina vimeripoti kuwa William Dodson, mwenye umri wa miaka 42, anakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela.
ENDELEA
Posted By: MJOMBA ZECODER

MATUKIO DUNIANI

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger