Kokeini yenye thamani ya bei ya
mtaani kiasi cha Euro 50 m imegundulika katika kiwanda cha a Coca-Cola
kilichopo kusini mwa Ufaransa.
![]() |
Wafanyakazi wa kiwanda cha Coca-Cola wamekataa kuhusishwa kama wachunguzi wa chanzo cha mihadarati hiyo |
Kukamatwa kwa kilo 370kg za kokeini kunafanya kiwango hicho kuwa kikubwa zaidi kuwahi kupatikana kwenye ardhi ya Ufaransa.
Mwendesha mashtaka mjini Toulon, Xavier Tarabeux, amesema kuwa bei ya mtaani ya dawa hiyo ya kulevya ni "Euro milioni 50" na kwamba ni tukio baya sana la kushangaza".
Wafanyakazi wa kiwanda cha Coca-Cola wamekataa kuhusishwa kama wachunguzi wa chanzo cha mihadarati hiyo .
" Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa wafanyakazi wa kiwanda hizo hawahusiki kwa vyovyote vile ," alieleza rais wa kikanda wa Coca-Cola Jean-Denis Malgras,
Mwezi Aprili 2015, maafisa wa forodha wa Ufaransa walisaidia katika kuwamakata wanaume wawili waliokamatwa walipokuwa wakijaribu kuendesha manuari iliyokuwa imesheheni kilo 250 za kokeini hadi Uingereza.
No comments:
Post a Comment