Wanawake watano waliovalia mabuibui
na walioaminika kuvaa mikanda ya kujilipua walivamia kituo kimoja cha
polisi mjini Mombasa katika shambulio la kigaidi.
Polisi wanasema kuwa washukiwa hao waliwasili katika kituo cha polisi cha Central ili kuripoti kuhusu simu ya rununu ilioibiwa.
Polisi wanasema kuwa waliwafyatulia risasi na kuwaua wote.
Maafisa waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini huku kituo hicho cha polisi kikilindwa ili kuhakikisha kuwa hakuna tishio jingine.
Kumekuwa na mashambulio kadhaa katika eneo la pwani ya Kenya katika miaka ya hivi karibuni mengi yakifanywa na kundi la kigaidi la al-Shabab.
No comments:
Post a Comment