15.09.2016
DRC: kalenda ya uchaguzi itaanza na uchaguzi wa urais
Uchaguzi wa rais, wa wabunge na wa mkoa utafanyika mbalimbali DRC. |
Ujumbe wa kambi ya upinzani ulikua unataka uchaguzi wa urais ndio
uanze. Uchaguzi huo utafanyika na chaguzi zingine tatu ikiwa kifedha na
kiufundi itawezekana.ENDELEA
10.09.2016
Washirika wa kisiasa wa Merkel wazidi kumtia kishindo
Merkel, ambaye umaarufu wake wa muda mrefu umeshuka kufuatia mgogoro wa
wakimbizi, siku ya Jumatano alivionya vyama vya siasa dhidi ya
kujishusha hadhi kwa kuchukuwa msimamo wa chama cha AfD wa kueneza chuki
dhidi ya Uislamu.ENDELEA
10.09.2016
Viongozi wa NATO, EU wazuru Uturuki
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akisalimiana na katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg mjini Ankara. |
Uturuki imekuwa ikitaka kujiunga na Umoja wa Ulaya kwa muda mrefu,
lakini imewatuhumu wazungu kwa kukwamisha mchakato huo kwa sababu ya
chuki dhidi ya taifa hilo la Kiislamu. Maafisa wa Umoja wa Ulaya
wanasema Uturuki bado haijatimiza masharti kuhusu haki za msingi na
uhuru.ENDELEA
09.09.2016
Korea Kaskazini yafanya 'jaribio kubwa la nyuklia'
Korea Kaskazini kufikia
sasa haijasema lolote kuhusu jaribio hilo, lakini wachanganuzi wanasema
hii huenda ikawa ishara ya hatua zilizopigwa na taifa hilo katika
kustawisha teknolojia yake ya nyuklia.
Mitetemeko ya ardhi ya kusababishwa na binadamu ambayo imetokea eneo hilo awali yote ilitokana na majaribio ya nyuklia.ENDELEA
Mitetemeko ya ardhi ya kusababishwa na binadamu ambayo imetokea eneo hilo awali yote ilitokana na majaribio ya nyuklia.ENDELEA
09.09.2016
Jean Ping wa Gabon kukata rufaa, mahakama ya rufaa
Bwana Ping amesema watu kadhaa wameuawa kwenye
vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi , lakini serikali imesema kuwa ni
watatu pekee ndiyo waliuawa.ENDELEA
09.09.2016
Obama:Trump hana ufahamu
Akizungumza
Laos, Bw Obama amesema kuwa kila mara Bw Trump anapoongea inabainika
kwazi kwamba mgombea wa Republican hafai kuwa rais.ENDELEA
07.09.2016
Rais Bongo awatuhumu waangalizi wa umoja wa Ulaya
Akizungumza
kupitia kituo cha taifa cha Redio cha RTL, Rais Bongo amesema kuwa,
angetamani kuona waangalizi hao pia wanagusia kasoro zilizoshuhudiwa
kwenye ngome za mpinzani wake wake, mjini Fiefdom.ENDELEA
07.09.2016
Amani yaanza kutengamaa Sudan Kusini
Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini
Salva Kiir amemtumia ujumbe Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki akimuarifu kuwa hali ya
usalama katika nchi hiyo imeanza kutengemaa.ENDELEA
05.09.2016
Merkel atikiswa uchaguzi mdogo Ujerumani
Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel ameonekana kutikiswa kisiasa huko kaskazini mashariki mwa jimbo la Mecklenburg-Pomerania.ENDELEA
05.09.2016
Wataamu wasema wizi wa kura barani Afrika waelekea kukoma
Wakati huu nchi ya Gabon ikikabiliwa na machafuko
ya mara baada ya uchaguzi mkuu ulioshuhudia kurejea madarakani kwa Rais
Ali Bongo Ondimba, wataalamu wanasema kuwa udanganyifu wa chaguzi barani
Afrika unazidi kuwa mgumu, shukrani kwa mashirika ya kijamii ambayo
yamekuwa yakifuatilia chaguzi mbalimbali na kukosoa pamoja na kuenea kwa
teknolojia ya simu za mkononi.ENDELEA
05.09.2016
Hakuna siri tena, Kenyatta asaini kuwa sheria muswada wa haki ya kupata taarifa
Muswada wa haki ya kupata
taarifa nchini Kenya wa mwaka 2015, hatimaye umetiwa saini na Rais kuwa
sheria, ukiruhusu raia wa Kenya kupata taarifa kwa uhuru kutoka
Serikalini pamoja na ofisi nyingine za uma.ENDELEA
05.09.2016
Obama na Xi Jinping waendelea kutofautiana kuhusu Bahari ya China Kusin
Hata
hivyo Rais Xi alipinga mpango wa Marekani wa kupeleka mfumo wa kuzuia
makombora katika anga huko Korea Kusini. Aliitaka Marekani kuheshimu
maslahi ya kimkakati na usalama ya China.
Kwa upande wake rais Obama wa Marekani alisisitiza kwamba nchi yake lazima ihakikishe usalama wa washirika wake.ENDELEA
Kwa upande wake rais Obama wa Marekani alisisitiza kwamba nchi yake lazima ihakikishe usalama wa washirika wake.ENDELEA
04.09.2016
Rais Robert Mugabe atoa mzaha kuhusu afya yake
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe
amepuuzilia mbali taarifa za hivi karibu za uvumi juu ya afya yake, kwa
kutoa mzaha kwamba alikufa na akafufuka.ENDELEA
04.09.2016
Kuapishwa rais mpya nchini Brazil katika anga ya mgogoro wa kisiasa na kiuchumi
Michel Temer, rais wa muda nchini Brazil amekula kiapo kama rais mpya wa nchi hiyo.
Mbali na Temer kuahidi kufanya juhudi kwa ajili ya kuokoa
uchumi wa Brazil kutokana na mdororo, amesisitiza pia kwamba, hivi sasa
na baada ya kuenguliwa madarakani Rais Dilma Rousseff, umefika wakati wa
kuiunganisha nchi hiyo. Katika hotuba yake ya kwanza kwa taifa na baada
ya kuapishwa,ENDELEA
04.09.2016
Uhuru akanusha mvutano kati ya Kenya na Tanzania
Akizungumza mjini Mombasa wakati wa ufunguzi gati la makontena katika
bandari ya Mombasa, Kenyatta alipuuzia maneno kwamba kuna mvutano
wowote na badala yake akasema kuwa nchi hizo zinasaidiana.ENDELEA
04.09.2016
Jean Ping ajitangaza rais nchini Gabon ataka kura kuhesabiwa upya
Watu watano wameuawa na maelfu kukamatwa katika makabiliano kati ya wafuasi wa upinzani na jeshi la polisi jijini Libreville.ENDELEA
02.09.2016
Uzbekistan 'waomboleza kifo' cha rais Islam Karimov
Watangazaji waandamizi wa runinga ya
taifa na viongozi wakuu wa serikali nchini Uzbekistan wametuma ujumbe
wa tanzia katika mitandao ya kijamii kufuatia kuzagaa kwa uvumi kuwa
rais Islam Karimov ameaga dunia.ENDELEA
02.09.2016
Melania Trump ashtaki gazeti kuhusu tuhuma za ukahaba
Melania Trump amelishtaki gazeti la
Daily Mail la Uingereza pamoja na mwanablogu wa Marekani akitaka alipwe
$150m (£114m) kuhusiana na tuhuma kwamba alikuwa kahaba miaka ya 1990,
wakili wake amesema.ENDELEA
02.09.2016
Mamia ya watu wakamatwa katika vurugu Gabon
Rais
Ali Bongo ambaye ndiye aliyetangazwa mshindi katika uchaguzi huo
amewalalamikia wafuasi wa upinzani ambao walimiminika mitaani siku ya
Jumatano na kuchoma moto bunge la nchi hiyo.
Amesema demokrasia haiwezi kupatikana kwa njia kama hizo.ENDELEA
Amesema demokrasia haiwezi kupatikana kwa njia kama hizo.ENDELEA
01.09.2016
Hatimaye Rousseff aenguliwa rasmi madarakan
Rais Mpya wa Brazil Michel Temer
amesema nchi yake inaingia katika enzi mpya ya matumaini baada ya
kuondoshwa madarakani kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Dilma Rousseff.ENDELEA
01.09.2016
Ukuta: Upinzani waahirisha maandamano Tanzania
Muungano wa vyama vya upinzani nchini Tanzania umeahirisha maandamano ya kitaifa ambayo yalikuwa yamepangiwa kufanyika kesho.
01.09.2016
Ali Bongo atangazwa mshindi wa uchaguzi Gabon
Wanachama wa tume ya Uchaguzi mkuu
nchini Gabon wametangaza kuwa rais Ali Bongo, amehifadhi kiti chake cha
urais baada ya kumshinda mpinzani wake Jean Ping.ENDELEA
31.08.2016
Hoja za mwisho kuhusu hatma ya rais Dilma Rousseff
Rais Rouseff anatuhumiwa kuivunja sheria ya bajeti mwaka
2014,ili kuficha hali mbaya ya kiuchumi inayokabili taifa hilo,tuhuma
alizokanusha vikali. Baraza la Senete linatazamiwa leo
kusikiliza hoja za mwisho kutoka kwa mawakili wa pande zote mbili, kabla
ya kikao cha mwisho ili kufanyika kura hiyo ya kuamua hatma ya rais
Rouseff. Kikao hicho kinatazamiwa kuendelea hadi kesho. Ili kumuondoa
madarakani rais Rouseff Thuluthi mbili au maseneta 51 miongoni mwa 81
wanapaswa kupiga kura kuunga mkono wazo hilo.ENDELEA
31.08.2016
Mmoja wa makamanda wa IS auawa nchini Syria
Kundi la wapiganaji la Islamic state
limetangaza kuwa mmoja wa kamanda wake mwandamizi ambae ni msemaji wa
kundi hilo, Abu Muhammad al-Adnani ameuwawa nchini Syria.ENDELEA
31.08.2016
Viongozi wa upinzani wa Chadema nchini Tanzania kuhojiwa zaidi na polisi
Polisi
waliwashikilia viongozi hao kufuatia kukiuka amri iliyotolewa na jeshi
la polisi mwishoni mwa juma lililopita kupiga marufuku mikutano yote ya
ndani ya vyama vya siasa.ENDELEA
30.08.2016
Serikali imetangaza kuzifunga stesheni 'zilizomtusi' Magufuli
Serikali ya Tanzania imetangaza
kuzisimamisha kwa muda stesheni mbili za redio ,radio 5 na Magic FM kwa
madai ya kumtusi rais Magufuli na kuchochea ghasia nchini.ENDELEA
30.08.2016
Maafisa wa Chadema wakamatwa Tanzania
Polisi nchini Tanzania wamewakamata maafisa wa chama kikuu cha
upinzani cha Chadema akiwemo mgombea wa zamani wa uraiswa chama hicho
Edward Lowassa.ENDELEA
30.08.2016
Maoni: Kansela Angela Merkel hajaamua juu ya kushiriki katika uchaguzi
Lakini mgogoro wa wakimbizi tangu mwaka uliopita umebadilisha kila
kitu.Hisia miongoni mwa wananchi zimegawanyika. Nusu ya wananchi bado
wanamwona Merkel kuwa ni kiongozi mzuri. Lakini wengine wanamkosoa, na
hata wanafikia hatua ya kuwa na mtazamo mkali juu yake. ENDELEA
30.08.2016
Rais wa Brazil Dilma Rousseff ajieleza baraza la Seneti
Dilma Rousseff akijieleza mbele ya Seneti |
Nje ya ukumbi wa seneti mamia ya wafuasi wa rais huyo wameonekana
wakiendesha magari yao huku wakipiga kelele za kutaka kurudishwa
madarakani pamoja na kuwa kuna matumani hafifu kwa Dilma kurejea katika
nafasi hiyo. Mmoja kati ya watu wanaoumuunga mkono kiogozi huyo anasemaENDELEA
Aug 29, 2016
Mgombea wa upinzani Gabon adai kushinda uchaguzi wa rais
Ping alisema jana kuwa
amechaguliwa na kwamba anamsubiri Rais anayemaliza muda wake amuite na
kumpongeza. Jean Ping ameyasema hayo siku mbili kabla ya kutangazwa
matokeo rasmi ya uchaguzi wa rais.ENDELEA
29.08.2016
Uchaguzi wa ushindani mkali kuwahi kushuhudiwa Gabon
Mpinzani mkuu Jean Ping. |
Wananchi wa Gabon Jumamosi (27.08.2016) wamejitokeza katika uchaguzi
atakaokuwa na ushindani mkali kabisa kuwahi kumkabili Rais Ali Bongo
ambaye familia yake imeidhibiti nchi hiyo kwa takriban nusu karne.
Bongo mwenye umri wa miaka 57 alishika madaraka hapo mwaka 2009 wakati baba yake Omar alipofariki dunia hapo mwaka 2009 baada ya kuwa madarakani kwa miaka 42 na alisdhinda katika uchaguzi mwaka huo huo.Vyombo vya dola na mitandao iiliyojikita yenye kumpendelea vyote hivyo vikililainishwa na utajiri wa mafuta wa nchi hiyo Bongo yumkini akashinda tena safari hii.ENDELEA
Bongo mwenye umri wa miaka 57 alishika madaraka hapo mwaka 2009 wakati baba yake Omar alipofariki dunia hapo mwaka 2009 baada ya kuwa madarakani kwa miaka 42 na alisdhinda katika uchaguzi mwaka huo huo.Vyombo vya dola na mitandao iiliyojikita yenye kumpendelea vyote hivyo vikililainishwa na utajiri wa mafuta wa nchi hiyo Bongo yumkini akashinda tena safari hii.ENDELEA
29.08.2016
Uturuki yazidisha mashambulizi ndani ya Syria
Waasi wanaoungwa mkono na Uturuki wamekabiliana na vikosi vinavyoungwa
mkono na Wakurdi kaskazini mwa Syria, huku jeshi la Uturuki likiendeleza
kampeni yake ndani ya ardhi ya Syria.
Kifaru cha Uturuki kwenye ardhi ya Syria. |
Serikali ya Uturuki, ambayo yenyewe inapambana na uasi wa Wakurdi ndani
ya ardhi yake, inasema kampeni yake nchini Syria inahusiana pia na
kuwazuwia Wakurdi kutwaa maeneo zaidi ndani ya Syria sambamba na
kuwarejesha nyuma wapiganaji wa kundi lijiitalo Dola la Kiislamu (IS).
Uturuki inataka kuwazuwia wapiganaji wa Kikurdi kujiimarisha ndani ya
Syria karibu na mpaka wake, jambo ambalo inahofia litakipa nguvu chama
cha Wakurdi, PKK, ambacho kimekuwa kwenye vita vya miongo mitatu sasa
kuwania utawala wake wa ndani.ENDELEA
26.08.2016
Uturuki yazidi kutuma vifaru Syria
Vifaru vyengine kumi vya Uturuki Alhamisi (25.08.2016) vimevuka mpaka
kuingia Syria siku moja baada ya wapiganaji wa upinzani wa Syria
wanaoungwa mkono na Uturuki kuwatimuwa wanajihadi katika mji wa
Jarabulus.
Vifaru hivyo vinatarajiwa kuungana na vile ambavyo vilivuka mpaka hapo
jana katika Operesheni Ngao ya Euphrates ambayo Uturuki inasema
inakusudia kuwatokemeza wanamgambo wa itikadi kali wa kundi la Dola la
Kiislam na wale wa KikurdiENDELEA
26.08.2016
Colombia yatangaza makubaliano ya kihistoria ya amani
Serikali ya Colombia na waasi wa kundi la FARC wametangaza kufikia
makubaliano ya mwisho kumaliza vita vya msituni vilivyodumu kwa miaka
50.Rais Barack Obama amempongeza mwenzake wa Colombia kwa mafanikio
hayo.
Pande hizo mbili zimesema zimefikia makubaliano kuhitimisha mgogoro na
kujenga amani, katika taarifa ya pamoja iliyosomwa na wawakilishi wa
Cuba na Norway, ambao ndiyo wapatanishi katika mazungumzo yaliyopelekea
kufikiwa makubaliano hayo.ENDELEA
24.08.2016
Msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania ataka mazungumzo, upinzani waonya
Msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania, jaji mstaafu Francis
Mutungi, ameingilia kati mvutano wa vyama vya siasa nchini Tanzania,
ambapo ametaka kufanyika kwa kikao cha pamoja kati yake na viongozi wa
vyama vya siasa kupata muafaka.
Msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania, jaji mstaafu Francis Mutungi |
Uamuzi wa msajili wa vyama kuingilia kati mvutano huu, imekuja baada ya
chama kikuu cha upinzani nchini humo, CHADEMA, kusisitiza azma yake ya
kufanya maandamano ya nchi nzima September mosi mwaka huu kupinga hatua
ya Serikali kukataza kufanya mikutano ya kisiasa.ENDELEA
24.08.2016
Majeshi ya Uturuki yaimarisha mashambulizi ngome ya IS, Syria
Kwa siku ya pili mfulululizo majeshi ya Uturuki yameendelea
kuyashambulia maeneo ya mpakani yanayodhibitiwa na wapiganaji wa dola la
kiislamu IS nchini Syria.
Binali Yildirim:Waziri mkuu wa Uturuki |
Hatua hiyo ni katika kuyajibu mashambulizi yanayofanywa na kundi
hilo la IS tukio la hivi karibuni likiwa mashambulizi ya makombora
mawili yaliyolenga mji wa Karkamis ulio kusini mashariki mwa Uturuki. ENDELEA
19.08.2016
Wafuasi 418 wa Ikhwanul Muslimin wahukumiwa adhabu kali na mahakama ya kijeshi ya Misri.
Mahakama ya kijeshi ya Misri imetoa hukumu ya vifungo vya kuanzia miaka
miwili hadi maisha jela kwa watu 418 ambao ni wanachama na wafuasi wa
harakati ya Kiislamu ya Ikhwanul Muslimin.
Mahakama hiyo imetoa hukumu kwa watu 350 bila ya wenyewe kuwepo mahakamani za kuanzia miaka 25 hadi kifungo cha maisha jela. Washtakiwa 68 waliokuwepo mahakamani wamehukumiwa vifungo vya kati ya miaka miwili hadi kumi jela.ENDELEA
19.08.2016
Picha ya mvulana wa Syria iliyowasikitisha wengi
Picha ya mvulana mdogo akiwa ameketi
kwenye gari la kubebea wagonjwa Syria, imeweka wazi tena madhila
wanayopitia raia nchini Syria.
Picha hiyo ya Omran, 4, imesambaa sana mtandaoni sawa na ilivyofanya picha ya mwili wa Aylan Kurdi, uliopatikana katika ufukwe wa Uturuki mwaka jana.ENDELEA
19.08.2016
UN:Riek Machar yuko DRC
Umoja wa Mataifa umesema Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Kusini Riek
Machar ambaye alikuwa haonekana hadharani yuko nchini Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Congo.
Taarifa zainasema Kikosi cha Majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa
Mataifa yaliyopo Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yalimsaidia yeye, mke
wake pamoja na wengine kutoka kwenye mpaka unaogawa nchi hizo mbiliENDELEA
UCHAGUZI WA URAISI ZAMBIA
Edgar Lungu ashinda
Rais wa Zambia Edgar Lungu ametangazwa mshindi wa matokeo ya uchaguzi wa urais kulingana na matokeo rasmi ya uchaguzi.Tume ya uchaguzi nchini Zambia imesema kuwa Lungu alijipatia asilimia 50.35 siku ya Alhamisi ,ikiwa imepita asilimia 50 inayohitajika ya kuzuia raundi ya pili kulingana na sheria mpya ya uchaguzi. Mpinzani wake Hakainde Hichilemi alijipatia asilimia 47.67 ya kura. Awali,chama chake cha UNPD kilijiondoa katika shughuli ya kuhakiki kura akidai kuwa kulikuwa na udanganyifu.
No comments:
Post a Comment