Most Popular

MASUALA YA KIJAMII

 

14.09.2016

Wabunge wataka matumizi ya bangi yahalalishwe Uingereza

 Wabunge hao wanataka serikali iondoe bangi kutoka kwa kitengo nambari moja hadi kitengo nambari nne.ENDELEA

 

12.09.2016

Waislamu kusherehekea Idd-el-Hajj 

 Barani Afrika sikukuu hii itasherehekea katika nchi mbalimbali, huku baadhi ya nchi zikiwa katika hali ya sintofahamu kutokana na makundi yanayodai kuwa yenye msimamo mkali wa kidini, hasa nchini Somalia, Nigeria, Mali, Libya, Mauritania na nchi nyingine za Kiarabu barani Asia, na Ulaya.
Kati ya Waislamu duniani sikukuu hii hujulikana kwa majina mbalimbali ambayo hutafsiriwa pia kwa lugha mbalimbali kama vile:ENDELEA

 

 

10.09.2016

Ri Chun-hee:mwanamke maarufu zaidi Korea Kaskazini  


Ndiye aliyetangaza vifo vya viongozi wa awali: Kim Il-Sung na Kim Jong-Il.
Ri Chun-hee majuzi alitangaza kufanikiwa kwa Korea Kaskazini kurusha satelaiti ya kuzunguka dunia kwa kutumia roketi. Hilo lilishutumiwa kama njama ya kufanyia majaribio kombora la masafa marefu.ENDELEA

 

09.09.2016 

Air China yaomba radhi baada ya kushtumiwa ubaguzi

 Shirika la ndege la China la Air China limeomba radhi baada ya kutuhumiwa kujihusisha na mambo ya ubaguzi kwa abiria wanaosafiri na ndege zake, na hivyo kulazimika kuondoa gazeti lake lililozua utata katika ndege zake.ENDELEA

 

09.09.2016 

Mzee wa umri wa miaka 145 Indonesia

 Mzee huyo anasema kwa sasa anaishiwa na nguvu na hawezi kutarajia aishi muda mrefu zaidi.
"Sina nguvu kama zamani. Hata kutembea ni shida. Nilikuwa mkulima na nilivua samaki mtoni. Sitaki kuendelea kuishi sana, ndio maana nimeandaa kaburi. "Ili nikifariki, kila kitu kiwe tayari," anasema.ENDELEA

 

05.09.2016

Biashara baina ya nchi za Afrika yasaidia kukuza uchumi

 Licha ya kuwa na ukuaji wa wastani wa mauzo ya nje wa asilimia 8.5 tangu mwaka 2010, fursa za kibiashara za kikanda hazijatumika kikamilifu barani Afrika. Hiyo ni kulingana na Ripoti ya hali ya Uchumi wa Afrika ya mwaka 2016 iliyotolewa Jumatano wiki iliyopita.
Ripoti hiyo inasema, biashara kati ya nchi za Afrika bado ni ya chini ikilinganishwa na sehemu nyingine za dunia.ENDELEA

 

 

05.09.2016

Mkutano wa kilele wa G20 kusaidia kuharakisha maendeleo ya viwanda Afrika

Mkutano wa 11 wa kilele wa kundi la G20 umefunguliwa leo huko Hangzhou, China, ambao umeshirikisha nchi nyingi zaidi zinazoendelea katika historia ya kundi la G20. Mkutano huo kwa mara ya kwanza umetoa kipaumbele kwa suala la maendeleo kwenye mfumo wa sera za dunia nzima, huku ukitoa pendekezo la ushirikiano linalolenga kuunga mkono maendeleo ya viwanda wa Afrika na nchi zilizo nyumba kimaendeleo duniani. Wachambuzi wanaona kuwa China kuweka ajenda hiyo kwenye mkutano huo na kuwaalika nchi za Afrika kuhudhuria mkutano huo kumeonesha kuwa China inazingatia suala la maendeleo la nchi za AfrikaENDELEA

 

 

05.09.2016

Utajiri wa Aliko Dangote washuka kwa zaidi ya asilimi 35

  Utajiri wa tajiri mkubwa zaidi barani Afrika raia wa Nigeria Aliko Dangote, umeshuka kwa asilimia 35 hadi kufikia kiwango cha dola za Marekani bilioni 9.9, kutokana na kushuka kwa thamani ya Naira na kuporomoka kwa bei ya madini katika soko la dunia, taasisi ya Bloomberg imesema.ENDELEA

04.09.2016

Kirusi cha Zika chahatarisha maisha ya watu bilioni 2 Afrika na Asia

 Uchunguzi umebaini kuwa, kirusi cha Zika kinahatarisha maisha ya watu zaidi ya bilioni mbili katika nchi kadhaa za mabara ya Afrika na Asia.ENDELEA

 

 03.09.2016

Iran na Tanzania kuimarisha uhusiano wa kiutamaduni

 

 Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeazimia kuimarisha uhusiano wa kiutamaduni na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.ENDELEA

 

31.08.2016

Saudi Arabia yafunga sHULE yake Ujerumani

Skuli ya King Fahd Academy mjini Bonn, Ujerumani, ambayo inamilikuwa na serikali ya Saudi Arabia itafungwa rasmi mwanzoni mwa mwaka 2017.
Serikali ya Saudi Arabia imeamua kuifunga shule yake ya pekee nchini Ujerumani, baada ya kulalamikiwa kwa muda mrefu kwamba huenda ikawa inatumika kupandikiza na kueneza siasa kali.

Ubalozi wa Ufalme wa Saudia mjini Berlin unasema skuli hiyo ifahamikayo kama King Fahd Academy iliyopo katika kiunga cha Bad Godesberg, karibu na mji mkuu wa zamani wa Ujerumani Magharibi, Bonn, itafungwa mwanzoni mwa mwaka ujao.ENDELEA

 

31.08.2016

IMF: Uchumi wa Tanzania waongoza Afrika Mashariki

 Katika ripoti yake iliyotolewa hii leo Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu cha ukuaji wa uchumi wake wa asilimia 6.9% mwaka wa 2016.ENDELEA

30.08.2016

EAC yaidhinisha kiswahili kuwa lugha rasmi

 Bunge la Afrika Mashariki limepitisha azimio la kuifanya lugha ya kiswahili kuwa lugha rasmi ya jamii ya Afrika Mashariki kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania.ENDELEA

 

 

 29.08.2016

Zimbabwe yakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji

Wanawake na watoto wakisubiri maji mjini Harare
 Zimbabwe ambayo zamani ilifahamika kama mzalishaji mkuu wa chakula barani Afrika inakumbwa na ukosefu mkubwa wa maji ambao unaweza kusababisha na ukame wakati nchi hiyo ikiwa inaelekea katika kipindi cha kiangazi.

Kutokana na ukosefu wa maji, wananchi nchini Zimbabwe sasa wanatembea mpaka umbali wa kilometa 15 kufatuta maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kunywesha mifugo yao kutokana na vyanzo vingi vya maji kukauka, yakiwemo mabwawa na visima.ENDELEA

26.08.2016

Utumwa mambo leo katika ajira

Wasichana wafanyabiashara nchini Ghana
Asilimia 60 ya mataifa yote duniani yapo katika hatari ya kutumia ajira ya utumwa mambo leo katika shughuli za uzalishaji licha ya kuwa suala hilo la kuwatumikisha watu katika ajira limekuwa likipingwa na wanaharakati.

Kulingana na ripoti mpya iliyotolewa hivi karibuni kuhusu viwango vya kutumikishwa watu katika ajira, Korea Kaskazini ndiyo nchi iliyo na rekodi mbaya zaidi ya kutumikisha watu katika ajira.

Utafiti uliofanywa na kampuni ya Verisk Maplecroft ikitumia vigezo vya visa vilivyoripotiwa vya usafirishaji watu kwa njia zisizo halali au utumwaDRC, sheria za nchi na utendaji wa vyombo vya dola katika nchi 198, kampuni hiyo imegundua kuwa nchi 115 ziko katika hatari ya kuwatumia watumwa.ENDELEA

 

24.08.2016

Hati za umiliki ardhi kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji nchini Tanzania

Nchini Tanzania kumekuwa na mzozo mkubwa wa matumizi ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji. Lakini juhudi za hivi karibuni za kutoa hati za umiliki wa ardhi zinaanza kutoa matunda katika kupunguza mizozo hiyo.
Mkulima wa mahindi Mkoani Morogoro nchini Tanzania
 Hali hii inaelezwa kuchangiwa na uandikishaji duni wa umiliki wa ardhi ambao kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na shirika uwazi la kimataifa yaani Transparency International 2014 Global Corruption mchakato wa upimaji nchini humo meghubikwa na rushwa.ENDELEA

 

23.08.2016

Madaktari wasio na mipaka kujiondoa Yemen

Shirika la madaktari wasio na mipaka jana lilisema litawaondoa wafanyikazi wake kutoka hospitali linazofadhili Kaskazini mwa Yemen baada ya watu 19 kuuawa katika shambulizi la angani dhidi ya Hospitali moja.

Wafanyikazi wa kimataifa wa msaada waondoka Sana'a baada ya uwanja wa ndege wa kimataifa kufunguliwa tena kwa mashirika ya msaada .
Muungano unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya waasi nchini Yemen hii leo umesema kuwa unataka kikao cha dharura na shirika la madaktari lisilokuwa na mipaka la -MSF- kuhusiana na hatua ya kutaka kuondoa wafanyikazi wake kutoka hospitali sita katika nchi hiyo inayokumbwa na ghasia.ENDELEA

 


Posted By: MJOMBA ZECODER

MASUALA YA KIJAMII

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger