Most Popular

Zaidi ya watu 300 wafariki dunia kwa mafuriko nchini India

Zaidi ya watu 300 wanaripotiwa kufariki dunia nchini India kufuatia janga la mafuriko yaliyotokea mashariki na katikati mwa nchi hiyo.

Duru rasmi za serikali ya India zinaripoti kwamba, mafuriko hayo yameharibu kabisa vijiji, mazao na barabara katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko hayo.

 Taarifa zaidi zinasema kwamba, mafuriko hayo yamesababishwa na mvua kubwa iliyoyakumba baadhi ya maeneo ya India na kwamba, watu milioni sita wameathiriwa na mafuriko hayo huku wengi kati yao wakiwa wamepelekwa katika kambi za misaada katika majimbo ya Madhya Pradesh, Bihar, Uttar Pradesh, Rajasthan na Uttarakhand.

Kikosi cha Taifa cha India cha Kukabiliana na Maafa kimetumwa katika majimbo yaliyokumbwa na mafuriko na kwamba, kimefanikiwa kuwaokoa raia 33,000.

Kikosi cha Taifa cha India cha Kukabiliana na Maafa kimetumwa katika majimbo yaliyokumbwa na mafuriko na kwamba, kimefanikiwa kuwaokoa raia 33,000.


 Jimbo la Bihar linaripotiwa kuwa na idadi ya watu wengi waliopoteza maisha katika mafuriko hayo baada ya viwiliwili 120 kupatikana hadi sasa, Shule zote zimefungwa katika jimbo la Uttar Pradesh na kwamba, watu 43 wamefariki dunia jimboni humo kufuatia mafuriko hayo

Aidha watu 70 wameaga dunia katika jimbo la Madhjya Pradesh tangu kuanza kwa mafuriko hayo na kwamba, nyumba nyingi zimesombwa na maji katika jimbo hilo.

Adha ya mafuriko India  

Maelefu ya watu wanaripotiwa kubakia bila makazi kutokana na nyumba zao kusombwa na mafuriko hayo.

India ni miongoni mwa nchi ambazo hukumbwa na mafuriko kila mwaka na mamia ya watu hupoteza maisha yao kutokana na janga hilo la kimaumbile.
Posted By: MJOMBA ZECODER

Zaidi ya watu 300 wafariki dunia kwa mafuriko nchini India

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger