Nchini Brazil, mwendesha mashitaka anayehusika na 
uchunguzi wa kashfa ya rushwa katika kampuni ya umma ya mafuta ya 
Petrobras, aliomba Jumatano, Septemba 14 kushtakiwa kwa rais wa zamani 
Lula kwa rushwa na kujitajirisha kinyume cha cheria.
![]()  | 
| Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva na mkewe Marisa Leticia Agosti 15, 2016 katika mji wa Sao Paulo | 
Haya ni mashambulizi ya moja kwa moja na mabaya zaidi kuelekezwa dhidi ya Lula. "Leo
 hii, Mwendesha mashitaka mkuu anamtuhumu Bw Luiz Inacio Lula da Silva 
kuwa kiongozi mkuu wa rushwa kuhusiana na uchunguzi uliyopewa jina la 
Lava Jato [uoshaji wa haraka], " amesema mwendesha mashitaka, Deltan Dallagnol.
Anamshutumu rais wa zamani wa mrengo wa kushoto kuwa ni "kiongozi mkuu wa uhalifu wa rushwa" unaohusiana na kampuni kubwa ya umma ya mafuta Petrobras, jina lililopewa kashfa hiyo ya rushwa iliyoibuka katika miaka mitatu iliyopita, lakini ingekuwa imeanza chini ya utawala wa Lula, wakati mwenyewe aliteua wakurugenzi wa kampuni ya Petrobras wanaohusika na kuhudumia mtandao mkubwa wa rushwa.
Kwa mujibu wa mwendesha mashitaka, ambaye amewakilisha faili hiyo katika mahakama kwa minajili ya kufunguliwa mashtaka yeye na mkewe Marisa Leticia, wawili hao wanahusika moja kwa moja na kashfa hii.
Lula anatambulika kama mkuu katika uongozi wa uhalifu, na ambaye alikua akiratibu utekelezaji wake. " Euro milioni moja ilitolewa katika neema yake, " kwa mujibu wa mwendesha mashitaka.
Kwa upande wa wafuasi wa rais wa zamani, shutuma hizi ni mbinu za kumkamata Lula, wiki mbili baada ya kuondolewa mamlakani Dilma Rousseff, ambalye alimrithi Lula katika uongozi wa nchi.

No comments:
Post a Comment