Most Popular

Jackie Chan kupewa tuzo ya Oscar ya staha

Mwelekezi na mwigizaji mashuhuri wa filamu Jackie Chan atapokea tuzo ya staha ya Oscar kwa mchango wake mkubwa katika tasnia ya filamu.

Licha ya umaarufu wake, Bw Chan hajawahi kushinda tuzo ya Oscar
Jopo linalotoa tuzo za Oscar pia limeidhinisha kutuzwa kwa mhariri Anne Coates, mwelekezi Lynn Stalmaster na mwandalizi wa filamu za makala Frederick Wiseman.

Rais wa jopo hilo Cheryl Boone Isaacs amewataja wanne hao kama "waasisi halisi na stadi katika kazi waliyoifanya".

Chan, 62, alikuwa mwigizaji nyota katika filamu nyingi za kung-fu zilizoandaliwa katika nchi yake ya kuzaliwa, Hong Kong.

Msururu wa filamu za Rush Hour ulivuma sana kimataifa
Alivuma kimataifa kwa filamu kama vile Rumble in the Bronx, Rush Hour na filamu ya vibonzo ya Kung Fu Panda.
Posted By: MJOMBA ZECODER

Jackie Chan kupewa tuzo ya Oscar ya staha

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger