Most Popular

Watu 500 waripotiwa kupoteza maisha yao kwa ugonjwa wa kipindupindu Kongo DR

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, jumla ya watu 500 wamepoteza maisha yao nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kutokana na ugonjwa wa kipindupindu.

Mgonjwa wa kipindupindu akiwahishwa hospitali
Taarifa iliyotolewa na shirika hilo sanjari na kuonyesha wasi wasi wake juu ya kuenea ugonjwa huo imesema kuwa, watu elfu 18 wameambukizwa maradhi hayo. Kadhalika limeongeza kuwa tangu ugonjwa huo ulipoibuka hadi sasa jumla ya watu 517 wamepoteza maisha.

Ni vyema kuashiria kuwa, maradhi ya kipindupindu yamekuwa yakiripuka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hususan katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo. Kwa mujibu wa duru za afya nchini humo tangu mwezi Agosti hadi sasa watu 13 wameambukizwa ugonjwa huo mjini Kinshasa, mji mkuu wa taifa hilo, huku  wawili wakiripotiwa kufariki dunia. Ugonjwa wa kipindupindu huambukiza kutokana na kunywa maji yasiyo salama ambapo huendana na mgonjwa kuharisha na kutapika.
Posted By: MJOMBA ZECODER

Watu 500 waripotiwa kupoteza maisha yao kwa ugonjwa wa kipindupindu Kongo DR

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger