Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis,
Jumapili ya Agosti 4, 2016, amemtangaza Mama Teresa kuwa mtakatifu,
akisifu kazi alizozifanya mjini Kolkata India, kwa ni zaidi ya ubinadamu
na upendo wa Mungu aliokuwa nao kwa kuwasaidia watu masikini.
Sherehe za kumtangaza Mama Teresa
kuwa mtakatifu zilifanyika kwenye ibada maalumu ya utakaso kwenye
uwanja wa St Peters, ikiongozwa na Papa Francis mbele ya waumini zaidi
ya laki moja waliohudhuria.![]() |
Mama Teresa akiwa nje ya makao makuu ya kituo cha misaada cha kanisa katoliki mjini Kolkata nchini India, picha ilipigwa siku chache kabla ya kufariki kwake September 5, 1997. |
Papa Francis amesema kuwa licha ya kumtangaza kama mtakatifu, bado ataendelea kubaki kuwa Mama Teresa kwa kanisa katoliki.
Akipasa sauti yake na maono yake kuwa “kanisa masikini kwa watu masikini” papa Francis ameelezea kasi za Teresa kama kielelezo cha usafi wa matendo ya Mungu kwa watu masikini.
![]() |
Papa Francis akiongoza moja ya ibada alizozifanya hivi karibuni, amemtangaza Mama Teresa kuwa mtakatifu |
“Hebu tuchukue tabasamu lake na kuliweka mioyoni mwetu na kuwapa wale ambao tutakutana nao njiani hasa wale ambao wana taabika.”
Papa Francis alitumia ibada hiyo pia kusifu msimamo wa Mama Teresa wa kupinga kitendo cha utoaji mimba “ambacho kilibainishwa na Mama Teresa kama mauaji” na kushinda tuzo la Nobel mwaka 1979.
Ibada hii maalumuj imefanyika siku moja kabla ya maadhimishi ya 19 ya kifo cha Mama Teresa mjini Kolkata, mji wa India ambako Teresa aliishi huko kwa karibu miongo minne akifanya kazi kwenye maeneo ya watu masikini zaidi.
No comments:
Post a Comment