Waziri Mkuu wa Uturuki Binali
Yildirim, alisema Jumapili hii Septemba 4 kwamba mpaka wa Uturuki na
Syria sasa uko salama kabisa na vikosi vya Uturuki vinadhibiti eneo
hilo. Kundi la Islamic State limepoteza maeneo iliyokua ikiyashikilia
hivi karibuni.
![]() |
Raia na vifaru vya jeshi la Uturuki katika mpaka wa Uturuki na Syria, Septemba 3, 2016. |
Kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya
miaka miwili, kundi la Islamic State limepoteza ngome zake zote kwenye
mpaka wa Uturuki na Syria. Mapigano mapya yaliyoanzishwa na jeshi la
Uturuki katika eneo la Al-Ain yalizaa haraka matunda, kwani
yalilazimisha wapiganaji wa kijihadi wa kundi la Islamic State
kukimbilia katika eneo la kusini, na hivyo kupelekea Uturuki kudhibiti
mpaka wake wa kusini na Syria, kuanzia eneo la Jarablos hadi Azaz.
Pamoja na kushindwa kushindwa huko, kundi la Islamic State limepoteza mawasiliano yoyote na makundi mengine washirika yalioko maeneo tofauti duniani. Kupoteza eneo hili la mpakani, litapelekea kundi hili kushindwakuajiri wapiganaji wapya na kupata chakula na vifaa vingine kutoka Uturuki.
Hatua ya tatu inafungua kama sehemu ya "Operesheni ya Shield Efrati." Sasa ni kwa jeshi la Uturuki na waasi wa Syria, aidha kuelekea kusini kwa lengo la kuuteka mji wa Al-Bab, moja ya ngome ya ngome za misho za kundi la Is katika mkoa wa Aleppo, aidha kuelekea katika mji wa Mambj ili kuwatimua wapiganaji wa Kikurdi.

No comments:
Post a Comment