Most Popular

Jeshi la Nigeria: Makamanda watatu wa Boko Haram wameuawa, kiongozi wao amejeruhiwa vibaya

Kiongozi wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram la nchini Nigeria inaaminika kuwa amejeruhiwa vibaya katika shambulio la anga lililofanywa na jeshi kaskazini mashariki mwa nchi. Hayo ni kwa mujibu wa duru rasmi za jeshi la nchi hiyo.
Abubakar Shekau, kiongozi wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram


Jeshi la anga la Nigeria limetangaza leo kuwa siku ya Ijumaa, ndege za kivita za jeshi hilo zilifanya shambulio kwenye msitu wa Sambisa. Msemaji wa jeshi, Kanali Sani Kukasheka Usman amesema makamanda watatu wa kundi hilo Abubakar Mubi, Malam Nuhu na Malam Hamman wameuawa; na kiongozi wao anayejulkana kama 'Abubakar Shekau' inaaminika kuwa amejeruhiwa vibaya mabegani.

Wanajeshi wa Nigeria

Hadi sasa kundi la Boko Haram halijatoa kauli yoyote kuhusiana na taarifa hiyo ya jeshi.
Kwa mujibu wa duru za habari, inasemekana shambulio hilo la jeshi la anga la Nigeria lilifanyika wakati wapiganaji wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram walipokuwa kwenye 'hafla fulani'.

Duru hizo zimeongeza kuwa shambulio la Ijumaa lililenga kambi ya Shekau ambako inaaminika ndiko wanakoshikiliwa wasichana zaidi ya 200 wanafunzi wa shule moja ya mjini Chibok waliotekwa nyara mwezi Aprili mwaka 2014 na kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram.

Taarifa ya jeshi la Nigeria imetolewa sambamba na kuwasili nchini humo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry ambaye atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa serikali ya Abuja yanayotazamiwa kukita zaidi kwenye suala la mapambano dhidi ya kundi la Boko Haram.

Katika miezi ya hivi karibuni, na kwa msaada wa vikosi vya nchi jirani za Chad, Cameroon na Niger, jeshi la Nigeria limefanikiwa kukomboa maeneo mengi ya ardhi ya nchi hiyo yaliyokuwa yakishikiliwa na kundi hilo la kigaidi na kitakfiri.../
Abubakar Shekau, kiongozi wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram       
Posted By: MJOMBA ZECODER

Jeshi la Nigeria: Makamanda watatu wa Boko Haram wameuawa, kiongozi wao amejeruhiwa vibaya

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger