Marekani imekubali kusambaza misaada
ya kijeshi nchini Israel ndani ya miaka 10 ijayo kwa mkataba wa dola
bilioni 38, mkataba huo ni mkubwa katika historia ya Marekani.
![]() |
Netanyahu alitembelea ngome ya jeshi la anga ya Israel mwezi Agosti |
Lakini Israel wanatakiwa kufanya makubaliano kadhaa na Marekani ya kupata fedha ikiwemo makubaliano ya kutochukua fedha za ziada kutoka Congress na kuahidi kuwa hawatatumia fedha za msaada kwa ajili ya ulinzi wake mwenyewe.
![]() |
Rais Obama na Netanyahu hawakutani mara kwa mara |
Maofisa wanasema kuwa Rais Obama na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wanaweza kukutana kwa mazungumzo katika mkutano mkuu wa umoja wa mataifa jijini New York.
No comments:
Post a Comment