Mkuu wa zamani wa Shirika la Kijasusi la Israel MOSSAD amesema, suala la kuundwa nchi huru la Palestina ni jambo lisiloepukika.
| Tamir Pardo, mkuu wa zamani wa Shirika la Kijasusi la Israel MOSSAD | 
Shirika la habari la Associated 
Press limemnukuu Tamir Pardo akisema hayo jana na kuongeza kuwa, suala 
la kuanzishwa nchi huru ya Palestina ni muhimu mno kwa usalama wa 
Mashariki ya Kati.
Matamshi hayo ya mkuu wa zamani wa 
shirika la kijasusi la utawala wa Kizayuni limeongeza idadi ya maafisa 
wa masuala ya usalama wa Israel ambao wanaamini kuwa amani haiwezi 
kupatikana Mashariki ya Kati bila ya kuundwa nchi huru ya Palesitna
Tamir Pardo amesema: Israel haiwezi 
kufikia makubaliano yoyote ya maana na ulimwengu wa Kiarabu bila ya 
kutatua kwanza kadhia ya Palestina
![]()  | 
| Mkuu wa zamani wa Shirika la Kijasusi la Israel MOSSAD amesema, suala la kuundwa nchi huru la Palestina ni jambo lisiloepukika. | 
Pia amesema, Benjamini Netanyahu, Waziri
 Mkuu wa utawala wa Kizayuni amepasisha pendekezo la kuundwa nchi huru 
ya Palestina, lililobakia sasa ni kumtaka atekeleze kivitendo tu 
pendekezo hilo.
Makumi ya makamanda wa zamani wa kijeshi
 na kiusalama wa Israel wamemtaka Benjamin Netanyahu afanye juhudi kubwa
 zaidi za kulipatia ufumbuzi suala la Palestina.


No comments:
Post a Comment