Uratibu wa mashirika ya kiraia
katika mkoa wa Tanganyika ulitangaza Alhamisi hii Septemba 8 kuwa
"shughuli zitasimama" katika mji wa Kalemie kwa kupinga dhidi ya
kukithiri kwa ukosefu wa usalama katika mji huo.
![]() |
Barabara kuu katika mkoa wa Tanganyika, DRC, Machi 25, 2016. |
Maduka mengi na masoko vilifungwa. Shughuli za uchukuzi na biashara zilizorota mchana kutwa katika mji wa Kalemi.
Mgomo huu ulifanyika kufuatia mauaji ya watu wawili Jumatano wiki hii katika kata ya Dav. Watu hao waliuawa kwa kupigwa risasi na watu wenye silaha wasiojulikana.
"Vifo vya watu wawili, hii ni dalili tosha ya kuongezeka kwa ukosefu wa usalama, " wamelaani viongozi wa mashirika ya kiraia mjini Kalemi. Viongozi wa mashiriaka ya kiraia wanawatuhumu viongozi wa mkoa wa Tanganyika kufumbia macho hali ya usalama mdogo inayoendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Tangayika, hasa katika mji wa Kalemi.
"Ni jambo lisilokubalika kwa muda kama ule, milio ya risase isikike, na watu wapoteze maisha, na kisha msaada wa polisi ufike umechelewa.
"Viongozi wajaribu, si tu kukabiliana na mdororo wa usalama, lakini pia madhara yake, " amesema Modeste Kabazi, msemaji wa shirika moja la kiraia katika mkoa wa Tanganyika.

No comments:
Post a Comment