Kundi la wapiganaji la Islamic state
 limetangaza kuwa mmoja  wa kamanda wake mwandamizi ambae ni msemaji wa 
kundi hilo, Abu Muhammad al-Adnani ameuwawa nchini Syria. 
![]()  | 
| Abu Muhammad al Adnani | 
Wanajeshi wa marekani wamethibitisha kuwa walikuwa wamemlenga Abu Muhammad al-Adnani lakini wanasema bado walikuwa wakichunguza matokeo ya shambulizi la anga la siku ya Jumanne katika mji wa Al-Bab, kaskazini mashariki ya jimbo la Allepo.
Marekani inamuelezea Abu Muhammad al-Adnani kuwa ni mpangaji mkuu wa mashambulizi ya nje ya I-S na imesema kuwa kifo chake kinaweza kuwa nukta muhimu ya kushindwa kwa kundi hilo.


No comments:
Post a Comment