Vikosi vya uokoaji vya majini vya
Italy vimesema vimeratibu uokoaji wa wahamiaji elfu sita na mia tano
katika bahari ya Mediterania siku ya jumatatu. Kwa mujibu wa vikosi
hivyo, hii ni oparesheni kubwa zaidi kuwahi kutokea katika miaka ya hivi
karibuni.
![]() |
Mmoja wa wahamiaji akimbeba mtoto wake wa siku tano kuelekea katika boti ya waokoaji |
Maelfu ya raia wa kiafrika, wengi wao wakitafuta maisha bora barani ulaya, mara nyingi husafirishwa katika madau ambayo hayana hadhi ya kuhimili mikiki mikiki ya bahari.
Katika msafara huo pia, kuna wakimbizi kutoka maeneo ya vita kama mashariki ya kati na Afghanistan. Wengi wao wamepoteza maisha yao.
No comments:
Post a Comment