Most Popular

MICHEZO




15.09.2016

Matokeo ya michezo ya UEFA iliyochezwa usiku wa leo 

 Manchester City wakiwa nyumbani wameibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Borussia Moenchengladbach, hatrick ya Kun Aguero na goli moja la Kelechi Iheanacho yalitosha kuipatia Man City alama tatu na kuwa timu ya pili kwenye msimamo wa kundi C ambalo linaongozwa na Barcelona.ENDELEA


15.09.2016

KLABU BINGWA BARANI ULAYA:Leicester & Mahrez  WAWASHA MOTO

Frikiki ya Riyad Mahrez ilipatikana baada ya Jamie Vardy kuangushwa akijibu shambulizi
Mabingwa hao wa Ligi ya Premia walionekana kucheza kwa ukomavu mkubwa na kuonyesha wana uwezo wa kushindana katika soka ya Ulaya.ENDELEA


 15.09.2016

KLABU BINGWA BARANI ULAYA:RONALDO NA MORATA WATIBUA SHEREHE YA WARENO 

 wafunga magoli mawili ndani ya dakika  5

 

Kumbu kumbu muhimu :

*Ronaldo amefunga magoli mengi zaidi yatokanayo na mpira upigwao moja kwa moja zaidi ya mchezaji mwingine yeyoye yule(12)katika mashindano ya klabu bingwa barani ulaya tangu msimu wa 2003-2004

*Real Madrid wameshinda mechi zao zote za ufunguzi katika uwanja wa Santiago Bernabeu (mara 10).

* Ronaldo amefunga magoli 3 katika mechi 3 ambazo amecheza dhidi ya Sporting Lisbon kwenye Klabu Bingwa barani ulaya.

*Katika mashindano ya Ulaya,Sporting Lisbon wameshindwa kushinda mechi hata moja katika michezo yote 14 waliyochezea Hispania (D3 L11).ENDELEA

15.09.2016

KLABU BINGWA BARANI ULAYA:MAN CITY YAIADHIBU Mönchengladbach

 Aguero atupia 3,Ihenacho asema nami nimo,Gundogan we acha tu

Kama vile haitoshi,kiungo wa Man City,Gundogan aliingia ndani ya eneo la hatari la Mönchengladbach akitaka kuonana na kipa wa timu hiyo,lakini Kramer,Kiungo wa Mönchengladbach aliamua kumuangusha mchezaji huyo tukio lililomzawadia kadi ya njano na kuipatia Man City penati mnamo dakika ya 27 ya mchezo huo!!Hakufanya kosa.....Aguero alitumbukiza penati hiyo upande wa kulia huku goli kipa akiangukia upande wa kushoto.Hivyo kuiandikia Man City goli la pili...ENDELEA

14.09.2016

KLABU BINGWA BARANI ULAYA:MSN WAANZA KWA KUFUNGA MAGOLI ZAIDI YA TIMU NYINGINE YEYOTE ILE

hii inaamisha kuwa MSN wamefunga jumla ya magoli 6 katika ufunguzi wa mashindano hayo ,idadi ya magoli ambayo hayakuweza  kufungwa na timu yeyote ile katika ufunguzi wa mashindano hayo.ENDELEA


 14.09.2016

KLABU BINGWA BARANI ULAYA:BAYERN YAIADHIBU Rostov 5-0

 Lakini alitoke mchezaji aitwaye Juan Benart toka benchi na kuongeza goli la tano katika dakika za majeuhi za kipindi cha pili.Hadi mwisho wa mchezo,Bayern 5, Rostov 0ENDELEA


14.09.2016
BACELONA YAIFUNZA MPIRA CELTIC,YAINTADIKA 7-0

Data Muhimu:

*katika historia ya Klabu Bingwa barani Ulaya,Barceloan wameandika ushindi wao mkubwa katika mashindano hayo.

*katika mechi mbili  walizocheza katika mashindano ya klabu bingwa barani ulaya,Barcelona wameifunga Celtic jumla ya magoli 13

*Neymar ni mchezaji wa kwanza kusaidia upatikanaji wa magoli 4 tangu Zlatan Ibrahimovic alipofanya hivyo akiwa na PSG mwaka 2012

*Lionel messi amefunga magoli matatu mara 6 katika historia ya mashindano hayo zaidi ya mchezaji yeyote yule kuwahi kutokea.

 

*Luis Suarez ameshiriki katika upatikanaji wa magoli 20 ya Barcelona kwenye mashindano ya Kombe la washindi barani ulaya katika mechi 20,akifunga 17 na kusaidia upatikanaji wa mengine 7ENDELEA


Afrika Mashariki yaomboleza kifo cha kocha wa muda mrefu James Siang’a.

 Atakumbukwa sana nchini Kenya kuwa miongoni mwa wachezaji bora wa timu ya taifa na klabu ya Gor Mahia na timu ya taifa miaka ya 60 na 70.ENDELEA

Barcelona yalazwa nyumbani na timu iliopanda daraja 

 Suarez aliingizwa baada ya bao la Gomez lakini Alavez ilijikakamua na kupata ushindi wake wa kwanza katika uwanja wa Nou Camp tangu mwaka 2000.ENDELEA

Man City wawazima Man U nyumbani Old Trafford

Kevin De Bruyne alifunga bao la kwanza la Man City dakika ya 15
 Kevin De Bruyne alifunga bao la kwanza la Man City dakika ya 15 alipovamia ngome ya Manchester United na kumpata mlinzi Daley akiwa usingizini.ENDELEA




10.09.2016
Arsene Wenger: Sitaki Jack Wilshere ahame Arsenal

Arsene Wenger amesema matumaini yake ni kwamba kiungo wa kati Jack Wilshere, ambaye kwa sasa ametumwa Bournemouth kwa mkopo, atasalia Arsenal maisha yake ya uchezaji.ENDELEA

10.09.2016
Mourinho: Man City watakuwa hatari bila Sergio Aguero

"Inakuwa vigumu zaidi. Sergio Aguero akiwepo basi unajua atacheza, na unajua watajipanga vipi."
Mourinho amesema mmoja kati ya Kelechi Iheanacho, Raheem Sterling na David Silva anaweza kuchezeshwa kama 'nambari tisa bandia' kwenye debi hiyo Old Trafford.ENDELEA

09.09.2016

Rashford aifungia timu yake mabao matatu akiichezea kwa mara ya kwanza 

 Kinda wa klabu wa Manchester United, Marcus Rashford, amefunga mabao matatu wakati akiichezea kwa mara ya kwanza timu yake ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 21, wakati walipoifunga Norway kwa magoli 6-1 kwenye mchezo wa kufuzu kombe la mataifa Ulaya kwa vijana chini ya miaka 21.ENDELEA


09.09.2016

Mathieu Flamini: Crystal Palace wamchukua kiungo wa zamani Arsenal

Crystal Palace wamemchukua kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal Mathieu Flamini, ambaye alikuwa amesalia kuwa ajenti huru baada ya kuruhusiwa kuondoka na klabu ya Arsenal majira ya joto.ENDELEA



09.09.2016

Rais wa kamati ya kimataifa ya Olympic, kuchunguzwa

 Polisi nchini Brazil wamesema kuwa wanahitaji kuongea na Rais wa kamati ya kimataifa ya Olympic, Thomas Bach, kuhusu kuhusika na mpango haramu wa kuuza tiketi kwenye michuano ya Rio iliyokamilika mwezi uliopita, ambapo polisi wamesema watamhoji kama shahidi, na si mtuhumiwa. ENDELEA

09.09.2016

 Fifa yazuia usajili Real Madrid na Atletico Madrid

 Timu ya Real Madrid imeielezea hatua hiyo kama ukiukwaji wa haki na imeeleza dhamira yake ya kukata rufaa zaidi, katika mahakama ya Usuluhishi ya Michezo ENDELEA

 05.09.2016

Aguero amefunga mabao matatu katika mechi tatu msimu huu na City ambao wako juu ya jedwali kwa kushinda mecho zote walizocheza. ENDELEA

  05.09.2016

Mambo muhimu kuhusu wachezaji 46 wanaocheza EPL kutoka Afrika

Ligi ya Uingereza imetoa orodha rasmi ya wachezaji 25 watakaochezea kila klabu ya Uingereza katika ligi kuu msimu wa mwaka 2016-17.ENDELEA

 

 05.09.2016

Rooney aandika rekodi mpya kucheza michezo England

 Rekodi hii inaipita ile ya David Beckham ambaye aliichezea timu ya Taifa la England mechi 115.

 

 

 05.09.2016

Taifa Stars yaaga mchujo wa AFCON kwa kichapo cha 1-0 dhidi ya Super Eagles

 Taifa Stars kwenye mchezo wake huo mwa mwisho kwenye kundi G ilipokezwa kipigo cha goli 1-0, goli ambalo lilifungwa dakika ya 77 na nyota wa Nigeria anayeichezea Man City ya England Kelechi Iheanacho.ENDELEA

 05.09.2016

Hamisi Kiiza ajiiunga na Free state Stars ya Afrika Kusini


Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Simba na Yanga, Hamisi Kiiza ameasajiliwa na klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini inayaoshiriki ligi kuu.ENDELEA

05.09.2016

AFCON 2017: Burkina Faso na Uganda wafuzu


Jumapili Septemba 4, 2016 timu za Burkina Faso na Uganda zimefuzu kwa hatua ya fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2017. Uganda itacheza michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1978, kufuatia ushindi wake wa bao 1-0 dhidi ya Comoro.
Burkina Faso, wenyewe, wameishia wa kwanza katika kundi hili la D baada ya ushindi dhidi ya Botswana (2-1).ENDELEA
03.09.2016

Iwapo atapatikana na hatia ,mchezaji huyo wa Argentina atapigwa marufuku ya mechi tatu na kukosa deby ya Manchester mnamo tarehe 10 mwezi Septemba.ENDELEA

03.09.2016

Gareth Bale: Sijali kupoteza taji la mchezaji ghali duniani


 Mchezaji wa Real Madrid Gareth Bale anasema kuwa hashtushwi na hatua ya kupoteza taji la kuwa mchezaji ghali zaidi duniani alilopoteza kwa Paul Pogba.ENDELEA

 03.09.2016

Yaya Toure awachwa nje ya kikosi cha vilabu bingwa


 Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola amemwacha nje kiungo wa kati wa timu hiyo yaya Toure katika kikosi chake cha kombe la vilabu bingwa Ulaya mwaka 2016-17.ENDELEA

 02.09.2016

Usajili uliofanyika siku ya mwisho barani ulaya

David Luis arejea Chelsea

David Luis amerejea Chelsea
 Vilabu vya soka barani ulaya vimefanya usajili wa kumarisha vikosi vyao katika siku ya mwisho ya usajili uliofungwa usiku wa kuamkia Septemba mosiENDELEA

02.09.2016

Brazil, Argentina zashinda kufuzu kombe la dunia 2018 

 Michezo ya kuwania kuzufu kwa fainali za kombe la dunia zitazofanyika nchini Urusi mwaka 2018, kwa ukanda wa Amerika kusini, zimechezwa usiku wa kuamkia leo.ENDELEA

31.08.2016

Rooney kustaafu soka ya kimataifa 2018

 Mshambuliaji nyota na nahodha wa Uingereza Wayne Rooney anatarajia kustaafu soka la kimataifa baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 itakayofanyika nchini Urusi.ENDELEA

30.08.2016

Fabregas akana kukosana na mkufunzi Conte

 

Kiungo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas amepinga madai kwamba alikosana na meneja wa klabu hiyo Antonio ConteENDELEA

 


30.08.2016

Asamoah Gyan arudi Uingereza

 Nahodha wa kikosi cha soka nchini Ghana Asamoah Gyan anatarajiwa kujiunga na klabu ya Reading kwa mkopo kutoka timu ya China Shanghai SIPG.ENDELEA



29.08.2016

RACITIK AIOKOA BARCELONA,REAL MADRID YASHINDA KWA MBINDE,ATLETICO MADRID MAJI SHINGONI HISPANIA.

 

"Tunatakiwa kuungana na kupata matokeo bora,kwa sababu tukiendelea hivi tutajikuta tunapigana kutoshuka daraja" alisema Antoine Griezman.ENDELEA


 26.08.2016
UEFA CHAMPIONS LEAGUE GROUPS
Barcelona USO KWA USO NA  Man City, Arsenal KUPAMBANA NA  PSG KWENYE MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU YA UEFA Champions League ENDELEA


 26.08.2016

SAMATA AIONGOZA GENK KUCHEZA EUROPA LEAGUE

 

Goli lililofungwa na Mbwana Samata mnamo dakika ya 2 ya mchezo liliiwezesha Timu ya Racing GENK ya Ubelgiji kufuzu kucheza katika mashindano ya Europa League Msimu huu,mara baada ya kuilaza timu ya Lokola pimotiva Zagreb kwa mabao 2-0.ENDELEA


 25.08.2016

Samatta akaribia kucheza makundi Europa League

    
Samatta alianza kuchezea timu ya taifa ya Tanzania 2011ENDELEA
 24.08.2016

TP Mazembe na MO Bejaia zafuzu hatua ya nusu fainali taji la Shirikisho

Timu za soka za Etoile du Sahel ya Tunisia, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MO Bejaia ya Algeria na FUS Rabat ya Morroco, zimefuzu katika hatua ya nusu fainali kuwania taji la Shirikisho barani Afrika.
   Hatua hii inakuja baada  ya kumalizika kwa mechi za hatua ya makundi siku ya Jumanne.

Mazembe wakicheza nyumbani mjini Lubumbashi, waliwafunga Yanga FC ya Tanzania mabao 3-1 na kumaliza kundi la A kwa alama 13.ENDELEA 

Olimpiki: Brazil yavuna dhahabu katika soka

Kwa kuubusu mpira na bao ambalo halitasahaulika, nyota mkubwa wa Brazil Neymar aliwapa wenyeji wa mashindano ya Olimpiki muda ambao hautasahaulika katika mashindano haya.

Brazil ilishinda medali ya dhahabu ya olimpiki katika soka jana Jumamosi (20.08.2016) kwa mikwaju ya penalti na kuishinda Ujerumani, ikiwa ni ushindi wake wa kwanza katika historia ya olimpiki na kuzusha hali ya furaha kubwa katika taifa hilo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na kisha kupigiana penalti ambapo Brazil ilishinda kwa mikwaju 5-4.ENDELEA 


  18.08.2016

BARCELONA YATWAA KOMBE LA SUPER CUP HISPANIA


      Arda Turan alifunga mara mbili kabla Lionel Messi Hajaongeza goli la tatu  wakati barcelona ikiifunga  Sevila Magoli 3-0 siku ya jumatano na kutwaa kombe la Super Cup la Hispania kwa jumla ya magoli 5-0 ENDELEA


              SPANISH SUPER CUP::BARCELONA YAITANDIKA SEVILLA 2-0

Luis Suarez na Munir El Haddadi walifunga katika kipindi cha pili na kuipa Barcelona ushindi wa mabao mawili kwa nunge dhidi ya Seviila katika mchezo wa kwanza wa Super Cup nchini Hispania.
Katika dakika ya 54,Arda Turan kwa kutumia kifua Alimtengea mpira Luis Suarez ambaye bila kufanya kosa alifunga goli na kuiweka timu yake mbele kwa goli moja.Turan alipokea mpira huo toka kwa Dennis Suares
ENDELEA

Manchester United wamnunua

Kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 23 amerejea miaka minne baada ya kuondoka United na kwenda Juventus kwa £1.5m mwaka 2012. Pogba, ambaye ametia saini mkataba wa miaka mitano, ameongeza, "Hii ndiyo klabu bora kwangu kutimiza kila kitu ambacho kimekutumainia." Meneja Jose Mourinho amesema mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa huenda akawa nguzo ya klabu hiyo kwa mwongo mmoja ujao. United watalipa mabingwa hao wa Italia euro 105m kumchukua Pogba, pamoja na nyongeza euro 5m (£4.5m) ambayo ni bonasi kwa kutegemea mafanikio yake pamoja na gharama nyingine
Posted By: MJOMBA ZECODER

MICHEZO

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger