Shirika la Upelelezi la Marekani FBI limetoa ripoti yake ya uchunguzi kuhusiana na jinsi mgombea urais nchini humo kwa tiketi ya chama cha Democratic, Hillary Clinton alivyotumia anuani binafsi ya barua pepe kwa ajili ya mawasiliano ya kikazi wakati alipokuwa Waziri wa mambo ya nchi za nje.
Mapema mwaka huu FBI walisema kuwa Hillary alipaswa kuwa mwangalifu zaidi katika kutunza nyaraka za siri. Hata hivyo shirika hilo la upelelezi limesema kuwa hakukuwa na mazingira ya kumshitaki mgombea huyo wa urais nchini Marekani. Vyama vyote vya Republican na Democratic vimekiri kuwa ripoti hiyo ya uchunguzi inadhihirisha jinsi FBI ilivyojali katika kufuatilia kashfa hiyo. Hillary Clinton hadi sasa anaongoza katika kura za maoni nchini humo dhidi ya mpinzani wake Donald Trump, anayegombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican.
No comments:
Post a Comment