Most Popular

Walanguzi 2 wa biringanya kutoka Burundi wauawa Rwanda

Walanguzi wawili wa biringanya raia wa Burundi wameuawa jana usiku upande wa Rwanda wa mpakani, kwa mujibu wa msemaji wa polisi wa Burundi, Pierre Nkurikiye.

Wafanya biashara wa bringanya wa Burundi wameathiriwa sana
Aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter kwamba tukio hilo lilitokea majira ya saa tisa na dakika arobaini kwa saa za Burundi karibu na kituo cha mpaka wa Ruhwa, na kutaja waliouawa kuwa na wanaume wawili Fidele Niyonkuru na Jeremie Nyabenda.

Mwezi Julai, Burundi ilipiga marufuku usafiri wa umma na biashara zozote za chakula na Rwanda kwa sababu za kiusalama.

Wakulima wa biringanya na nyanya katika mkoa wa kaskazini magharibi mwa Burundi wa Cibitoke wameathirika pakubwa na uamuzi huo kwani Rwanda lilikua soko kuu la bidhaa zao.

Uhusiano baina ya Burundi na Rwanda umekuwa ukiendelea kuzorota tangu mwaka jana , huku serikali ya Bujumbura iskishutumu serikali ya Kigali kuwahifadhi waliopanga njama ya mapinduzi ya mwaka 2015 na kutoa zana na mafunzo ya kijeshi kwa warundi wanaoishi kambini nchini Rwanda.

Rwanda inapinga shutuma hizo inazosema hazina msingi wowote.
Posted By: MJOMBA ZECODER

Walanguzi 2 wa biringanya kutoka Burundi wauawa Rwanda

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger