Most Popular

Satelaiti ya Facebook ya kufikisha mtandao kasi Afrika yaharibiwa

Mwanzilishi wa kampuni ya Facebook Mark Zuckerberg amelezea kusikitishwa kwake baada ya satelaiti ambayo Facebook ingeitumia kwa mawasiliano ya kasi ya mtandao wa intaneti barani Afrika kuharibiwa.

Roketi ya Falcon 9 ilipolipuka
Satelaiti hiyo iliharibiwa katika mlipuko uliotokea eneo la Cape Canaveral jimbo la Florida, Marekani siku ya Alhamisi.

Satelaiti hiyo kwa jina Amos-Six ilikuwa imebebwa na roketi ya Falcon Nine ambayo ililipuka ilipokuwa ikifanyiwa majaribio ya kujiandaa kwa safari ya siku ya Jumamosi.
Mlipuko huo ulitokea wakati roketi hiyo ilikuwa ikijazwa mafuta na kutikiza majengo yaliyokuwa umbali wa kilomita kadha.

Mfanyakazi katika kituo jirani cha Kennedy Space Center alipiga picha ya mlipuko huo
Bw Zuckerberg, ambaye yumo ziarani Afrika, amesema "nimesikitishwa sana" kusikia kwamba satelaiti hiyo iliharibiwa.

Roketi ya Falcon-9 ilikuwa imeundwa ikiwa na uwezo wa kutua baharini au ardhini ikirejea duniani
"Tutaendelea kujitolea katika lengo lengo la kufikisha huduma ya mtandao kwa kila mtu na tutatia bidii hadi kila mtu apate nafasi na manufaa ambayo yangetokana na satelaiti hii," aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Posted By: MJOMBA ZECODER

Satelaiti ya Facebook ya kufikisha mtandao kasi Afrika yaharibiwa

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger