Safari ya miezi saba ya bajaji
inayotumia kawi ya jua na nguvu za umeme, ambayo ilikuwa inatoka India
kwenda hadi Uingereza, imesitishwa kwa muda baada ya wezi kuiba hati ya
kusafiria ya dereva wa gari hilo karibu na mji wa Paris.
Kwa sasa anasubiri kupata pasipoti mpya ndipo aweze kuvuka English Channel na kuhitimishia safari yake katika Kasri la Buckingham.
Bw Rabelli anajaribu kuwahamaisha watu kutumia kawi mbadala.
"Nimekuwa safarini kwa miezi saba sasa, na nimekuwa na hamu kubwa ya kufika Uingereza. Nimejiandaa kwa hili kwa miaka minne," ameambia BBC.
"Inaniuma sana kupoteza pasipoti yangu na euro 1,000" nikiwa safarini kuelekea Calais ambapo ningeabiri feri na kuingia Uingereza, amesema.
![]() |
Bw Rabelli akiwa na walinzi wa mpakani |
Amepitia Iran, Uturuki, Ugiriki, Bulgaria, Serbia, Austria, Ujerumani na Uswizi.
Huwa analala kwenye bajaji hiyo anapokosa mtu wa kumpa malazi.
Amefanikiwa kuweka akipa pesa nyingi kwa njia hii.
Mwanamume huyo wa miaka 35 ni mkazi wa India lakini ni raia wa Australia na amekuwa akifanyia kazi kampuni ya kuunda magari ya kutumia umeme nchini India, Mahindra Reva.
Alinunua bajaji hiyo $1,500 (£1,120) na akatumia $11,500 kuifanyia ukarabati.
Kwa sasa, bajaji yake inaweza kufikia kasi ya juu ya 60km/h (37 mph) ana hutumia umeme na kawi ya jua.
![]() |
Aiwa nje ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Alexander Nevski mjini Sofia, Bulgaria |
Gari hilo lake lina kitanda na jiko la sola.
No comments:
Post a Comment