Most Popular

Askofu wa Uingereza akiri kuwa ni shoga



Askofu Nicholas Chamberlain wa Grantham nchini Uingereza amekiri kuwa ni shoga, na kwamba Askofu Mkuu wa nchi hiyo alijua suala hilo kabla ya kumteua kuwa askofu.

Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby
Askofu Nicholas Chamberlain amesema amekuwa shoga kwa muda mrefu na kwamba amekuwa na mahusiano ya kingono na mwanaume mwenzake.

Chamberlain anakuwa askofu wa kwanza wa Kanisa la Uingereza (Church of England) kukiri kwamba ni shoga na amelazimika kukiri baada ya gazeti la Sunday kutishia kwamba, litafichua na kuanika wazi tabia hiyo.

Vyombo vya habari vinasema, suala hilo yumkini likazusha makelele mengi kati ya wafuasi wa kanisa hilo nchini Uingereza.

Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby amekubali kwamba alikuwa na habari kwamba askofu Nicholas Chamberlain ni baladhuli na shoga na kwamba alimteua kuwa askofu kutokana na umahii wake.

Gazeti al The Guardian la Uingereza limeandika kuwa, katika siku za hivi karibu maaskofu wengi wa Uingereza wamefunga ndoa na mashoga wenzao.
Posted By: MJOMBA ZECODER

Askofu wa Uingereza akiri kuwa ni shoga

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger