Kanda ya video mjini Paris
ilioonyesha mkahawa mmoja ukikataa kuwahudumia wanawake wawili Waislamu
imezua hisia kali nchini Ufaransa.
Kisa hicho kilitokea katika mkahawa wa Le Cenacle,Tremblay-en-France siku ya Jumamosi usiku.
Siku ya Jumapili,mtu huyo aliomba msamaha kwa kundi lililokongamana nje ya mkahawa huo.
Anasema kuwa alijisahau na kutoa matamshi hayo kutokana na mjadala unaoendelea nchini humo kuhusu vazi la Burkini katika fukwe za bahari za Ufaransa,na kwamba ana rafikiye aliyefariki katika shambulio la mjini Paris katika eneo la Bataclan mnamo mwezi Novemba.
Waandamana kupinga hatua ya mkahawa mmoja kukataa kuwahudumia wanawake Waislamu Ufaransa |
No comments:
Post a Comment