29.08.2016
Afrika katika magazeti
Buhari awavunja moyo vijana
Gazeti la "Neues Deutschland" linasema katika makala yake kwamba Rais
Muhammadu Buhari wa Nigeria aliekuwa mwakilishi wa matumaini makubwa,
amewavunja moyo vijana wa nchi yake.
Gazeti hilo linaeleza kwamba uchumi wa Nigeria,ambao ulikuwa unaongoza
barani Afrika sasa unarudi nyuma, wakati idadi ya watu wasiokuwa na
ajira inazidi kuongezeka. Thamani ya sarafu ya Nigeria, Naira pia
inaendelea kushuka.Vijana wa nchi hiyo wanahisi kuwa wamewekwa kandoni
mwa jamii.
Vijana waandamana nchini Nigeria ENDELEA |
Uturuki yaendelea kugonga vichwa vya habari
Mapambano dhidi ya wanamgambo wa dola la Kiislam IS,hali nchini Uturuki na hali ya kiuchumi nchini Marekani ni miongoni mwa mada zilizotangulizwa mbele na wahariri wa magazeti hii leo.
Hali nchini Uturuki inaendelea kugonga vichwa vya habari nchini Ujerumani. Mamilioni walikusanyika jana mjini Istanbul kulaani njama iliyoshindwa ya mapinduzi. Gazeti la "Landeszeitung" linaandika:"Hivyo ndiyyo siku ya suluhu inavyokuwa,ikiwa imeitishwa na chama pekee tawala AKP. Ingawa chama hicho kinachoongozwa na Erdogan kimekataza watu wasipepee bendera za vyama vya kisiasa,ili kutovuruga azma ya kudhihirisha mshikamano wakati wa kongamano hilo mjini Istanbul. Nia hiyo lakini haikufuatwa kikamilifu. Ingawa kujitokeza Erdogan na viongozi wa upinzani Kilicdaroglu na Bahceli ni ushahidi kamili kwamba upande wa upinzani na serikali wanalaani njama ya mapinduzi ya kijeshi. Hata hivyo kwa kutojumuishwa chama kinachoelemea upande wa wakurd,HDP katika kongomano hili pia,ni ushahidi kwamba azma ya mshikamano ni ya kijuu juu. Ukweli ni kwamba Uturuki inasalia kuwa nchi iliyogawanyika. Kwa upande mmoja imedhihirika jinsi mamilioni ya wananchi walivyopania kuona wanajeshi hawanyakui madaraka na demokrasia inalindwa. Na kwa upande mwengine lakini Erdogan anatawala kwa kupitisha kanuni bila ya kutilia maanani demokrasia.
No comments:
Post a Comment