Mhubiri wa Kiislamu mwenye msimamo mkali wa kidini
 Anjem Choudary, alihukumiwa Jumanne miaka mitano na nusu gerezani na 
mahakama ya London kwa kosa la kutoa wito wa kuunga mkono wanajihadi wa 
kundi la Islamic State (IS).
![]()  | 
| Anjem Choudary, London tarehe 31 Oktoba 2009 | 
Kelele za Allah Akbar ( "Mungu ni
 Mkubwa"), zilizotolewa na wafuasi wake hamsini zimesikika katika ukumbi
 wa mahakama wakati uamuzi huo ulipokua ukitsomwa. Anjem Choudray, 
mwenye asili ya Pakistan ambaye ni mwanasheria, ni Mubiri wa kihistoria 
katika jamii Jamii ya Waislamu nchini Uingereza. Mhubiri huyu mwenye 
umri wa miaka 49alitoa wito wa kuunga mkono kundi la Islamic State 
katika mfululizo wa video zilizorushwa hewani katika mtandao wa You 
Tube. Katika mahubiri yake,alikula kiapo kushirikiana na kundi la 
Islamic State na mara kwa mara alikua akiimba nyimbo zinazomsifu 
kiongozi wake Abu Bakr al-Baghdadi.
Tangu miaka ya 1990, alionekana mwanaharakati mkubwa katika masuala ya dini alipokua akiandamana mbelea ya Misikiti ofisi za balozi mbalimbali na vituo vya polisi nchini Uingereza. Alijukina sana na viongozi pamoja vyombo vya habari kutokana na maandamano hayo. Lengo lake kuu, amekua akisema Anjem Choudary, ilikua kupandisha bendera ya Kiislamu kwenye 10, Downing Street, makazi ya waziri mkuu.
Choudary ni mmoja wa vigogo wakuu wa kundi la Waislamu wenye msimamo mkali wa kidini wanaoendesha harakati zao nchini Uingereza. Aliwahi kuongoza shirika la Kiislamu la Al-Muhajiroun, ambalo pia linajulikana kama "Islam4UK" katikati ya miaka ya 2000.

No comments:
Post a Comment