Hatimaye Rais wa Marekani Barack Obama amekutana
na mwenzake wa Ufilipino, Rodrigo Duterte nchini Laos baada ya rais huyu
kumtusi kuwa ni “mwana wa kahaba”. Awali mkutano kati ya marais hawa
wawili ulifutiliwa mbali.
![]() |
Rais wa Marekani Barack Obama, akiwasili Laos, katika uwanja wa ndege wa Vientiane, Septemba 5, 2016. |
Mzozo Kati ya Obama na Dulerte
ulianza wakati Obama alibaini kwamba angemuuliza kiongozi Rais Rodrigo
Dulerte maswali kuhusiana na mauaji ya kiholela ya watu wanaotuhumiwa
kuhusika katika ulanguzi wa madawa ya kulevya nvchini Ufilipino.
Kiongozi wa Ufilipino Rodrigo Duterte amesema hakukusudia kumtusi Rais Barack Obama. Awali Rais Dulerte alisema anajutia kuona amatamshi yake kumhusu kiongozi wa Marekani Barack Obama yamefasiriwa kama matusi.
Bw Duterte alisema hayo baada ya Rais Barack Obama kufuta mkutano wake na kiongozi huyo kutokana na maneno ya lugha chafu yaliyoelekezwa kwake.
Kiongozi huyo wa Ufilipino alikuwa amemweleza Bw Obama kama "mwana wa kahaba" na kuongeza kwamba hatakubali kuulizwa maswali kuhusu ukiukwaji wa haki za kibinadamu nchini mwake.
Alisema Ufilipino haitawaliwi na mtu yeyote. Ufilipino ilikuwa koloni ya Marekani. Bada ya kashfa hiyo, Bw Obama alifuta mara moja mkutano wake na rais Dulerte.

No comments:
Post a Comment