Naibu wa rais nchini Afrika Kusini
alichukua fursa bungeni wakati ambapo rais wa taifa hilo Jacob Zuma
alikuwa amesafiri nje ya nchi kuwakilisha maswala ya serikali ikiwemo
kondomu isiyo na kelele na yenye ladha ya machungwa kwa wabunge.
![]() |
Naibu rais nchini Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akizundua mipira ya Kondomu bungeni |
Tangazo hilo la Ramaphosa lilizua hasira na tabasamu kutoka wanachama wa ANC na kelele kutoka kwa upinzani wa chama cha EFF huku baadhi ya wanachama wake wakisema ''mpatie Zuma hizo''.
Matamshi hayo ya wanachama wa EFF yanatoka miaka 10 iliopita wakati bwana Zuma alipokiri kwamba katika kesi yake ya ubakaji ,alifanya mapenzi bila kutumia mipira ya kondomu na mwanamke aliyekuwa na virusi vya HIV.
Aliondolewa mashtaka hayo lakini kukiri kwake kulizua mshangao mkubwa nchini humo ambapo takriban watu milion saba wana virusi
No comments:
Post a Comment