Most Popular

Teknolojia

 

12.09.2016

Roboti yafanya upasuaji wa macho mara ya kwanza duniani

 

Mgonjwa kwa jina Bill Beaver mwenye umri wa miaka 70 aliyefanyiwa upasuaji huo sasa anasema anahisi vyema.ENDELEA

 

 

10.09.2016

Galaxy Note 7: Wanaosafiri kwa ndege watahadharishwa  

 Kampuni ya Samsung ilisitisha uuzaji wa simu hizo na kukubali kwamba kulikuwa na hitilafu wakati wa uundaji wa betri za simu hizoENDELEA

 

09.09.2016 

Simu mpya ya Apple iPhone 7 isiyo na headphone za kawaida

Apple imesema kuondoa tundu hilo la headphone ya 3.5mm kutanusuru nafasi inayoweza kutumiwa kuongeza vitu vingine

 

Kampuni ya Apple imethibitisha kwamba simu yake mpya ya iPhone haitakuwa na tundu la kawaida la kifaa cha kusikiza sauti, ambacho kwa Kiingereza hufahamika kama headphone.ENDELEA

 

07.09.2016

TV za Sony Bravia kuathiriwa na mabadiliko ya Youtube

 Kutokana na hatua hiyo programu ya You Tube katika runinga hizo itaondolewa kufikia mwisho wa mwezi huu,Sony imesema.ENDELEA

 

04.09.2016

CHINA  KUFUNGUA DARAJA LA VIOO LILILO JUU YA ARDHI

Daraja la vioo lililojengwa juu nchini Uchina ililosifiwa kwa kuvunja rekodi lilipozinduliwa siku 13 tu zilizopita limefungwa. ENDELEA

03.09.2016

Samsung yasitisha uuzaji wa Note 7 sababu ya betri

 

  Mtu mmoja katika YouTube, anayesema anaishi Marekani, aliweka mtandaoni video inayoonesha Galaxy Note 7 ikiwa imeungua na skrini yake kuharibika.ENDELEA

03.09.2016

Satelaiti ya Facebook ya kufikisha mtandao kasi Afrika yaharibiwa


Roketi ya Falcon-9 ilikuwa imeundwa ikiwa na uwezo wa kutua baharini au ardhini ikirejea duniani
 Satelaiti hiyo kwa jina Amos-Six ilikuwa imebebwa na roketi ya Falcon Nine ambayo ililipuka ilipokuwa ikifanyiwa majaribio ya kujiandaa kwa safari ya siku ya Jumamosi.
Mlipuko huo ulitokea wakati roketi hiyo ilikuwa ikijazwa mafuta na kutikiza majengo yaliyokuwa umbali wa kilomita kadha.ENDELEA

 

02.09.2016

Acer yazindua laptopu yenye kioo kilichojipinda

 

 Kampuni ya Acer imezindua laptopu ya kwanza ilio na kioo kilichojipinda.Acer inasema kuwa uvumbuzi huo utaiwezesha kucheza michezo ya video.ENDELEA

01.09.2016

Rekodi ya kasi ya mtandao wa 4G katika simu yavunjwa

 

 Kampuni ya Finland Elisa inasema imefanikiwa kupata kasi ya Gigabait 1.9 kwa sekunde, ikisema hiyo ndio kasi ya juu zaidi kuwahi kupatikana.ENDELEA

29.08.2016

Iran kujenga vinu viwili vipya vya nyuklia

Kinu cha nyuklia cha Arak, nchini Iran

 

 Msemaji wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran aidha amesema, miswada ya mikataba ya kukifanyia ukarabati wa kimsingi kinu cha maji mazito ya nyuklia cha Arak imeshaandikwa. Ameongeza kuwa, mikataba hiyo itakuwa na mambo mengi ya kila namna ambayo yanahitajia vikao na mazungumzo mbalimbali kuyajadili.ENDELEA

 26.08.2016

Japani, Marekani kukuza nishati mbadala Afrika

 Japani na Marekani zimesaini makubaliano juu ya ushirikiano katika kuendeleza uzalishaji wa nishati ya joto ardhi barani Afrika.

Chini ya makubaliano hayo, serikali za nchi hizo mbili zitakuza uwekezaji kwenye vyanzo vya nishati vilivyo rafiki kwa mazingira barani humo. Nchi hizo mbili zitalenga katika maendeleo ya uzalishaji wa nishati ya joto ardhi katika eneo la Afrika Mashariki.

Ni asilimia 30 tu ya watu barani Afrika wanaotumia nishati ya umeme. Kuhakikisha upatikanaji wa vyanzo vipya vya nishati imekuwa ni suala linalohitajika haraka kutokana na uchumi wa eneo hilo kukua.
  ENDELEA 

26.08.2016

Sayari inayofanana na Dunia yagunduliwa

Wanasayansi wamegundua sayari ambayo inakaribia sana Dunia kwa mazingira na ukubwa wake na ambayo inazunguka nyota ijulikanayo kama Proxima Centauri, iliyo na mfumo unaokaribia zaidi mfumo wetu wa jua.
Proxima Centauri inavyoonekana kwa kutumia darubini ya Hubble Space Telescope
Sayari hiyo, ambayo kwa sasa imepewa jina 'Proxima b' inazunguka nyota hiyo katika eneo ambalo kuna uwezekano mkubwa sana wa kupatikana kwa maji.

Proxima inapatikana umbali wa kilomita trilioni 40 na inaweza kumchukua mtu, akitumia teknolojia ya sasa ya vyombo vya usafiri wa anga za juu, maelfu ya miaka kufika huko.ENDELEA

 

 

Simu milioni 900 za Android hatarini

Upungufu wa usalama wa herufi za siri za takriban simu milioni 900 umewapa wadukuzi fursa ya kudhibiti simu za android kote duniani. Upungufu huo unaowapa wadukuzi mlango wa nyuma wa kuiga herufi za siri uligunduliwa baada ya watafiti wa hali ya ubora wa programu Checkpoint walipojaribu kusuluhisha hitilafu iliyowezesha kirusi kuambukiza makumi ya mamilioni ya simu zilizokuwa na programu zilizoundwa na kampuni moja ya Marekani Qualcomm
ENDELEA
Posted By: MJOMBA ZECODER

Teknolojia

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger