Most Popular

Athari ya Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya

Juni 23 Uingereza ilipiga kura ya kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya EU katika kura ya maoni iliyofanyika nchini humo. Katika uchambuzi wa habari utamsikia Hidetoshi Nakamura Profesa mshiriki wa Chuo Kikuu cha Waseda katika kitivo cha sayansi ya siasa na uchumi, akizungumzia matatizo yanayoweza kujitokeza baada ya Uingereza kujiondoa EU pamoja na vile kujiondoa huko kunaweza kuathiri maeneo mengine.

“Ninaamini wananchi wengi wa Uingereza walichagua kujiondoa EU kutokana na ukosoaji usiokuwa na uwiano dhidi ya Umoja huo, unaoonekana kama moja ya miungano iliyoimarika zaidi.

Kwa mfano, suala la wahamiaji liliibua wasiwasi wa jamii katika nchi mbalimbali. Kwa uhakika, serikali kuu au za maeneo za kila nchi zinatakiwa kushughulikia suala la wimbi la wahamiaji. Wanatakiwa kujiandaa katika kuwakubali wahamiaji, kama vile kubadili mifumo yao ya hifadhi za jamii.

Pia ni kawaida kwa maoni ya nchi inayotoa mkopo na Umoja wa Ulaya kuwa Ugiriki ama nchi nyingine inatakiwa kupata udhamini ikiwa tu itafanya mabadiliko ya kibajeti na kuchukua hatua kali za kubana matumizi.

Lakini masuala haya yalipopelekwa kwenye siasa za ndani, EU ililengwa kirahisi kwa kulaumiwa kisiasa huku serikali za nchi wanachama zikishindwa kufahamu udhaifu wao.

Sera na mifumo iliyobuniwa kuwa kama kinga kwa bara la Ulaya zikikosolewa bila sababu. Hiki ni kitu ambacho kinatokea sio tu kwa Uingereza lakini ni kwa nchi nyingi wanachama wa EU. Kujiondoa kwa Uingereza kwenye Umoja huo kuliweka wazi madhara ya jumuiya ya eneo.

Lakini pia ni kweli kwamba upigaji kura wa Uingereza umekuja kwa sababu EU ina mfumo uliorasimishwa wa hali ya juu. Kwa maana hiyo miungano ya kimaeneo kama vile ile ya nchi za Kusini Mashariki mwa Asia ASEAN na Umoja wa Afrika AU ambayo haina mfumo uliorasimishwa kama ule wa EU, kwa sasa haina uwezekano wa kukumbana na ukosoaji kutoka nchi wanachama ama kuwa kwenye hatari ya kuvunjika.

Kwa sasa tukio baya kufuatia Uingereza kujiondoa EU ni ongezeko la migongano kati ya jamii ya Uingereza pamoja na watu wa mataifa mengine wanachama wa Umoja wa Ulaya. Kwa hiyo Umoja wa Ulaya ukiiwekea Uingereza vikwazo vikali kwa sababu ya kujiondoa kwenye umoja huo, itazidi kuleta chuki zaidi kwa raia wa Uingereza.

Kwa hiyo ninashauri Umoja wa Ulaya usimame kwa muda na kufikiri njia ya kukuza ushirikiano wa Ulaya huku ikiendeleza mkakati wake kama jumuiya kwa kuhakikisha amani na usalama ambazo zimejengwa kwa juhudi za zaidi ya miaka 70”.

Huo ulikuwa uchambuzi wa habari kutoka kwa Profesa mshiriki Hidetoshi Nakamura wa chuo kikuu cha Waseda katika kitivo cha sayansi ya siasa na uchumi.

         
Posted By: MJOMBA ZECODER

Athari ya Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger