Sheria kuhusu namna wasichana wa
shule za sekondari wanavyochana nywele nchini Afrika Kusini
zimesitishwa baada ya maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi
yaliyofanywa na wanafunzi weusi, ameleza waziri nchini humo.
![]() |
Wanafunzi katika shule ya sekondari ya Pretoria wanasema kuwa mara kwa mara waalimu huwaambia wanyooshe nywele zao na hawaruhusiwi kuzitengeneza katika mtindo wa Afro. |
![]() |
Picha ya mmoja wa waandamanaji iliyosambazwa kwa maelfu ya watu kwenye Twitter |
Sheria za shule zitasitishwa huku uchunguzi huru ukifanyika kuhusiana na madai hayo, amesema waziri wa elimu katika mkoa wa Gauteng.
Shule ya sekondari haijatoa kauli yoyote.
Kanuni kuhusu maadili ya shule hiyo ina orodha ya sheria kuhusu nywele, lakini haijataja mtindo wa nywele wa afro.
No comments:
Post a Comment