Idadi ya watu waliofariki kutokana
na tetemeko la ardhi katikati mwa Italia mapema Jumatano imefika 247
huku manusura wakiendelea kutafutwa.
Tetemeko hilo la nguvu ya 6.2 katika vipimo vya Richter liliharibu vibaya miji ya Amatrice, Accumoli na Pescara del Tronto ambapo watu wengi walifariki
![]() |
Nyumba nyingi Pescara del Tronto ziliporomoka |
Maafisa wa uokoaji waliendelea na juhudi za kuwatafuta manusura usiku, lakini wakati mmoja walitatizwa na mitetemeko mingine iliyotokea na kutikisa majumba yaliyosalia yakiwa bado wima.
Eneo lililokumbwa na tetemeko hilo ni milimani katika majimbo ya Umbria, Lazio na Marche.
![]() |
Manusura eneo la Amatrice wakesha chini ya mti usiku |
Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa karibu na Norcia, kilomita 170 kaskazini magharibi mwa mji mkuu Roma.
Mahema yamewekwa kuwasaidia watu walioachwa bila makao.
No comments:
Post a Comment