Most Popular

Watu kadhaa wauawa katika gereza la Qilinto



Habari ambazo hazijathibitishwa na serikali ya Ethiopia zinasema kwamba sisasi nyingi zilifyatuliwa Jumamosi Agosti 3 katika gereza lenye ulinzi mkali, lililo karibu na mji mkuu, Addis Ababa. Inaarifia pia kuwa moto uliwashwa katika gereza hilo.

Mtazamo wa mji wa Addis-Abeba, mji mkuu wa Ethiopia.
Kuna taarifa zinazosema kuwa moto huo uliwashwa kwa makusudi na wafungwa ambao walitaka kutoroka, lakini taarifa hii hayakuthibitishwa vyombo husika mjini Addis Ababa.

Taarifa kutoka vyombo vya habari nchini Ethiopia zinasema kuwa, watu wasiopungua 20 waliuawa katika mkasa huo, uliozuka katika gereza la Qilinto, ambako wanazuiliwa wafungwa wengi wa kisiasa.

Ethiopia imeendelea kukumbwa na hali ya sintofahamu, hasa maandamano na mauaji, ambako kila kukicha miili ya watu waliouawa imekua ikiokotwa katika maeneo mbalimbali. Hivi karibuni kulikua na maadamano yaliyojumuisha makabila makuu nchini humo.

Wanasiasa wengi wakiwemo wafuasi wa upinzani wanazuiliwa katika jela mbalimbali nchini humo. Wanaharaki wengi wa haki za binadamu nchini Ethiopia wamekua wakiishtumu serikali kukandamiza wapinzani na wale wote wanaothubutu kuikospa serikali ya nchi hiyo.
Posted By: MJOMBA ZECODER

Watu kadhaa wauawa katika gereza la Qilinto

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger