Mchezaji wa Real Madrid Gareth Bale
anasema kuwa hashtushwi na hatua ya kupoteza taji la kuwa mchezaji ghali
zaidi duniani alilopoteza kwa Paul Pogba.
![]() |
Gareth bale na Paul Pogba |
Gharama hiyo ya uhamisho iliipita ile ya Bale aliyehamia kutoka Tottenham Hotspurs hadi Real Madrid kwa takriban pauni milioni 85.3.
''Sijali kupoteza taji hilo'',alisema Bale,ambaye yuko na kikosi cha Wales kinachojiandaa kwa mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia siku ya Jumatatu nyumbani dhidi ya Moldova.
Huku Wales ikilenga kushiriki katika kombe la dunia la kwanza tangu mwaka 1958,Bale pia anatumai kuwa mchezaji wa sita nchini kwao kushinda kombel la Ulaya pamoja na lile la vilabu bingwa nyumbani.
No comments:
Post a Comment