![]() |
Wachezaji wa Madrid wakishangilia ushindi |
Ligi ya klabu bingwa barani ulaya
imeendelea kutimua vumbi usiku wa kuamkia leo ambapo kulikuwa na michezo
tisa ikipigwa katika viwanja tofauti.
Tottenham Hotspurs ikiwa nyumbani ilikubali kipigo cha 2-1 dhidi ya Monaco ya Ufaransa ambayo inaongoza ligi kuu nchini humo.
Lakini usiku wa kuamkia leo ilikuwa ni kicheko kwa wachezaji na washabiki wa Leicester City, wakiwa ugenini waliipiga Club Brugge ya ubelgiji jumla ya magoli 3-0 huku Riyad Mahrez akifunga mara mbili.
![]() |
Huu ni mchezo wa kwanza kwa Leicester City UEFA |
Borussia Dortmund ikiwa ugenini iliidhalilisha Legia Warszawa ya Poland kwa dozi ya 6-0.
Na katika mchezo uliowastaajabisha wengi ulikuwa ni mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya Sporting CP Lisbon ya ureno ambapo Madrid iliibuka na ushindi wa magoli 2-1.
Sporting Lisbon ilikuwa ya kwanza kuandika goli kwenye dakika ya 48 goli lililodumu hadi dk ya 89 ya mchezo ambapo C.Ronaldo aliisawazishia timu kwa mpira wa adhabu ndogo maridadi kabisa uliyoenda moja kwa moja kimiani, sekunde chache kabla mpira kumalizika Alvaro Morata aliiandikia Real Madrid goli la pili akiunganisha krosi ya James Rodriguez.
![]() |
Sergio Aguero kwa sasa ana magoli 9 katika michezo tisa ya msimu huu |
Matokeo mengine
Bayern 04 Leverkusen 2-2 CSKA Moscow
FC Porto 1-1 F.C. Copenhagen
Juventus 0- 0 Sevilla
Lyon 3-0 Dinamo Zagreb
No comments:
Post a Comment