18.08.2016
Arda Turan alifunga mara mbili kabla Lionel Messi Hajaongeza goli la tatu wakati barcelona ikiifunga Sevila Magoli 3-0 siku ya jumatano na kutwaa kombe la Super Cup la Hispania kwa jumla ya magoli 5-0.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa uturuki,alifunga goli la kwanza katika dakika ya kumi mara baada ya kupokea pasi toka kwa Lionel Messi kabla hajafunga goli la pili tokea mbali dakika mbili tu baada ya mapumziko.
wachezaji wa barcelona wakipongezana mara baada ya Arda Turan Kufunga Goli.
Katika dakika ya 55,Lionel messi aliongeza goli la tatu,Goli lililohitimisha jumla ya magoli 3-0 yaliyofungwa katika mchezo huo.
Barcelona walilazimika kumaliza wakiwa 10 uwanjani mara baada ya Javier Mascherano kuomba kutoka uwanjani dakika 10 kabla ya mpira kumalizika ili hali kocha wa timu hiyo,Luis Inlique ameshabadilisha wachezaji wote watatu wanaotakiwa kubadilishwa katika mchezo mmoja.<br>
Lilikuwa kombe la 8 KATI ya 10 ambayo Barcelona wangeweza kuchukua chini ya kocha Luis Enlique.
"Nahisi kuwa na bahati kuwa na wachezaji hawa.hawaachi kunishangaza .Tunataka kushinda makombe yote tuwezayo kushinda.unaliona hilo kwenye juhudi za wachezaji wangu" alisema Luis Enlique
No comments:
Post a Comment