![]() |
Aguero |
Alikuwa ni Segio Aguero!!mshambuliaji huyo hatari raia wa Ajentina aliiongoza timu yake kuiangamiza Borussia Mönchengladbach nchini Uingereza.Shoo ilianza katika dakika ya 8 ya mchezo pale Aleksandar Kolarov alipotupia majaro hatari ndani ya boksi la Mönchengladbach,mpira uliopokelewa vema na Aguero naye bila kufanya makosa akampeleka kipa sokoni na kuandika bao la kwanza.
![]() |
Ilkay Gundogan na Guadiola |
Kama vile haitoshi,kiungo wa Man City,Gundogan aliingia ndani ya eneo la hatari la Mönchengladbach akitaka kuonana na kipa wa timu hiyo,lakini Kramer,Kiungo wa Mönchengladbach aliamua kumuangusha mchezaji huyo tukio lililomzawadia kadi ya njano na kuipatia Man City penati mnamo dakika ya 27 ya mchezo huo!!Hakufanya kosa.....Aguero alitumbukiza penati hiyo upande wa kulia huku goli kipa akiangukia upande wa kushoto.Hivyo kuiandikia Man City goli la pili.....
HAKURIDHIKA!!Mnamo dakika ya 77 ya mchezo huo,Aguero alitupia goli lake la tatu kwenye mechi hiyo mara baada ya Sterling kumtengenezea nafasi safi,nae akamzunguka Sommer,kipa wa Mönchengladbach na kukutana na lango tupu la timu hiyo,nae bila kufanya kosa akatumbukiza mpira ndani ya nyavu na kufanya Man City kuwa mbele kwa magoli matatu kwa bila!!
![]() |
Ihenacho |
Alikuwa na mshambuliaji kinda wa timu hiyo,raia wa Nijeria,Ihenacho,aliyechukua nafasi ya mkongwe Sergio Aguero mnamo dakika ya 83 ya mchezo huo.Kinda huyo hakufanya makosa...mnamo dakika ya 90 + 1,ndani ya mda wa ziada na mpira ukielekea ukingoni pale alipotupia goli lake la kwanza katika mashindano hayo na kufanya ubao kusomeka 4-0.
Hadi mwisho wa mchezo,Man City 4, Mönchengladbach 0.
"Ni siku kamili kwangu"alisema Gundogan,mchezaji aliyeipatia Man City penati."Kusubiri mda mrefu halafu ukapea nafasi na kuonesha mchezo mzuri ni jambo zuri sana"alisema mchezaji huyo.
No comments:
Post a Comment