Most Popular

LA LIGA29

RACITIK AIOKOA BARCELONA,REAL MADRID YASHINDA KWA MBINDE,ATLETICO MADRID MAJI SHINGONI HISPANIA.

 

Ni wiki y a pili ya mshiake mshike nchini hispania katika ligi kuu ya soka nchini humo.Ni wiki iliyoshuhudia miamba ya soka nchini humo ikipata ushindi mwembamba kwa taabu sana kama si kuambulia sare.

IVAN Rakitic aiokoa Barcelona

ilikuwa ni katika dakika ya 20 ambapo kiungo wa kimataifa wa Croatia,İvan Rakitik alipoifungia Barcelona gol pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya timu ya Athletic Bilbao.Rakitic alifunga goli hilo mara baada ya kupokea pasi toka kwa Arda Turan aliyepokea mpira toka kwa Luis Suarez.

Hakuwa na bahati!!Luis Suarez alikosa goli la wazi mara baada ya mpira aliopiga kuokolewa ukiwa kwenye msitari wa goli katika dakika za majeruhi.hadi mwisho wa mchezo,Barcelona 1,Athletic Bilbao 0.

Real Madrid 2 Celta Vigo 1

Toni Kroos alifunga zikiwa zimesalia dakika tisa tu mpira kumalizika na kuihakikishia Real Madrid ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Celta Vigo. 

Alvaro Morata aliifungia real madrid goli la kwanza mnamo dakika ya 30 kabla Orellana hajaisawazishia Celta mnamo dakika ya 67.hadi mwisho wa mchezo,Real Madrid 2 Celta Vigo 1.

HAKUNA MBABE KATI YA ATLETICO MADRID NA Leganes
Haikuwa rahisi kwao hata kidogo.Atletico Madridi walijikuta wakikusanya poinkatit mbili tu  
katika michezo miwili waliyocheza mara baada ya kubanwa mbavu na timu ya Leganes,timu iliyopanda daraja msimu huu.

Kurudi kwa mshambuliaji wao matata,Antoine Griezman hakukuisaidia timu hiyo kuwaangusha vijana hao wapya katika ligi hiyo.

"Tunatakiwa kuungana na kupata matokeo bora,kwa sababu tukiendelea hivi tutajikuta tunapigana kutoshuka daraja" alisema Antoine Griezman.

Posted By: MJOMBA ZECODER

LA LIGA29

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger