Kwa kuubusu mpira na bao ambalo halitasahaulika, nyota mkubwa wa Brazil
Neymar aliwapa wenyeji wa mashindano ya Olimpiki muda ambao
hautasahaulika katika mashindano haya.
Brazil ilishinda medali ya dhahabu ya olimpiki katika soka jana Jumamosi (20.08.2016) kwa mikwaju ya penalti na kuishinda Ujerumani, ikiwa ni ushindi wake wa kwanza katika historia ya olimpiki na kuzusha hali ya furaha kubwa katika taifa hilo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na kisha kupigiana penalti ambapo Brazil ilishinda kwa mikwaju 5-4.
Kabla ya mkwaju wa mwisho wa penalti kwa Brazil, Neymar aliuchukua mpira na kuubusu na kuuweka katika alama ya penalti.
Kwa kusita kwanza, na kisha mkwaju safi, kwa utulivu aliuelekeza mkwaju wake wavuni na kisha alipiga magoti kabla ya kuvamiwa na wenzake kwa furaha.
Waandika historia
"Imekuwa" alisema Neymar. " Tumeandika historia."
Ulikuwa ushindi ambao ni zaidi ya soka kwa taifa hilo, ambalo lilikuwa linahitaji mno kitu cha kusherehekea.
Brazil imevurugwa na mdororo wa uchumi, kashfa za kisiasa, matatizo ya kiafya kuhusiana uchafuzi wa maji na virusi vya Zika na maswali kuhusiana na iwapo itaweza kuwa mwenyeji wa michezo ya olimpiki.
Matatizo yote hayo yalisahaulika wakati mkwaju wa Neymar ulipotinga wavuni.
herehe kubwa zilizuka katika mji wa Rio, ikiwa ni karibu na sherehe zilizofanyika kufuatia vikombe vitano vilivyonyakuliwa na Brazil katika kombe la dunia katika taifa hilo lenye wazimu wa soka.
Fashifashi zilionekana angani kuzunguka uwanja wa Maracana , honi za magari zilisikika na mashabiki waliimba na kupongezana na kumwagiana bia.
Wakati timu hiyo iliposimama katika jukwaa la kukabidhi medali , huku medali za dhahabu zikining'inia shingoni mwao , machozi yalibubujika katika nyuso za Wabrazil wakati uwanja wa Maracana ukihanikiza sauti za mashabiki wakiimba wimbo wa taifa.
Ushindi huo unakuja miaka miwili baada ya kipigo cha kudhalilisha cha mabao 7-1 nyumbani dhidi ya Ujerumani katika timu ya wakubwa katika nusu fainali ya kombe la dunia.
Brazil pia ilikuwa inajitoa kutoka katika kutolewa na mapema katika awamu ya makundi ya kombe la mwaka huu la mataifa ya bara la America, Copa America, na ilikuwa katika hali isiyokuwa na uhakika katika duru za mwanzo za kombe la Olimpiki.
Brazil ilishinda medali ya dhahabu ya olimpiki katika soka jana Jumamosi (20.08.2016) kwa mikwaju ya penalti na kuishinda Ujerumani, ikiwa ni ushindi wake wa kwanza katika historia ya olimpiki na kuzusha hali ya furaha kubwa katika taifa hilo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na kisha kupigiana penalti ambapo Brazil ilishinda kwa mikwaju 5-4.
![]() |
kikosi cha brazil kilichoshiolnda mashindano ya olimpiki |
Kwa kusita kwanza, na kisha mkwaju safi, kwa utulivu aliuelekeza mkwaju wake wavuni na kisha alipiga magoti kabla ya kuvamiwa na wenzake kwa furaha.
Waandika historia
"Imekuwa" alisema Neymar. " Tumeandika historia."
Ulikuwa ushindi ambao ni zaidi ya soka kwa taifa hilo, ambalo lilikuwa linahitaji mno kitu cha kusherehekea.
Brazil imevurugwa na mdororo wa uchumi, kashfa za kisiasa, matatizo ya kiafya kuhusiana uchafuzi wa maji na virusi vya Zika na maswali kuhusiana na iwapo itaweza kuwa mwenyeji wa michezo ya olimpiki.
Matatizo yote hayo yalisahaulika wakati mkwaju wa Neymar ulipotinga wavuni.
herehe kubwa zilizuka katika mji wa Rio, ikiwa ni karibu na sherehe zilizofanyika kufuatia vikombe vitano vilivyonyakuliwa na Brazil katika kombe la dunia katika taifa hilo lenye wazimu wa soka.
Fashifashi zilionekana angani kuzunguka uwanja wa Maracana , honi za magari zilisikika na mashabiki waliimba na kupongezana na kumwagiana bia.
Wakati timu hiyo iliposimama katika jukwaa la kukabidhi medali , huku medali za dhahabu zikining'inia shingoni mwao , machozi yalibubujika katika nyuso za Wabrazil wakati uwanja wa Maracana ukihanikiza sauti za mashabiki wakiimba wimbo wa taifa.
Ushindi huo unakuja miaka miwili baada ya kipigo cha kudhalilisha cha mabao 7-1 nyumbani dhidi ya Ujerumani katika timu ya wakubwa katika nusu fainali ya kombe la dunia.
Brazil pia ilikuwa inajitoa kutoka katika kutolewa na mapema katika awamu ya makundi ya kombe la mwaka huu la mataifa ya bara la America, Copa America, na ilikuwa katika hali isiyokuwa na uhakika katika duru za mwanzo za kombe la Olimpiki.
No comments:
Post a Comment