Kiungo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas amepinga madai kwamba alikosana na meneja wa klabu hiyo Antonio Conte.
Cesc Fabregas |
Fabregas hatahivyo amechapisha katika mitandao ya kijamii akisema kuwa wawili hao wana uhusiano mzuri na kwamba ataendelea kuichezea Chelsea.
''Mbali na ilivyoandikwa, mkufunzi Conte hajawahi kuniambia kwamba niondoke '',aliandika Fabregas.
Mkufunzi wa Chelsea Conte |
''Aliniambia kwamba ananitegemea na mimi namtegemea.Nitaendelea kuichezea klabu hii hadi mwisho na iwapo nitahitajika nitajitolea''
No comments:
Post a Comment