Most Popular

KLABU BINGWA BARANI ULAYA::BARCELONA 7,CELTIC 0

Brendan Rodgers alidhani Celtic walianza vema dhidi ya Barcelona ,lakini mwisho wa mchezo alielezea mechi hiyo kama moja  ya mechi waliyopoteza kwa uchungu.

Magoli matatu toka kwa Lionel Messi,Mawili toka kwa luis Suarez ,moja likifungwa na Neymar na jingine kupachikwa kimiani na Iniesta yalitosha kuizamisha Celtic katika usiku usiosahaulika kwa timu hiyo.

kwenye uwanja wa Camp Nou,Messi aliipatia Barcelona goli la kuongoza katika dakika ya tatu kabla Moussa Dembele hajapoteza nafasi ya dhahabu ya kufanya matokeo yawe 1-1 pale penati aliyopiga ilipookolewa na Marc-Andre ter Stegen.

 

akielezea penati waliyokosa,Rodgers alisema ulikuwa na mda muhimu katika mechi hiyo,ambapo kila kitu kiliharibika baada ya hapo.

"Ndiyo,hakuna utaalamu  katika hilo"alisema"nadhani katika kipindi cha kwanza,tulicheza vizuri na uelewano mkubwa tu"alimalizia Rodgers.

Ter Stegen AKİOKOA penati ya Dembele

"Tulipoteza goli mapema mdo katika mchezo huu,jambao ambalo nadhani silo unalotaka kufanya hapa.Lakini baadae tulirejea katika mchezo na kuanza kutengeneza nafasi za kufunga.Lakini ni wazi kuwa tulijua kuwa itakuwa vigumu kucheza na timu yenye umiliki bora wa mpira duniani,mara baada ya kucheza mechi iliyopita dhidi ya Rangers mwishoni mwa wiki.

Posted By: MJOMBA ZECODER

KLABU BINGWA BARANI ULAYA::BARCELONA 7,CELTIC 0

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger