Mshambuliaji nyota wa kimataifa wa
Tanzania, Mbwana Samatta leo anatarajiwa kuingoza klabu yake ya KRC Genk
ya Ubelgiji katika mchezo wa marudiano wa mwisho kuwania nafasi ya
kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya Europa League dhidi ya Lokomotiva
Zagreb ya Croatia .
![]() |
Samatta alianza kuchezea timu ya taifa ya Tanzania 2011 |
Wakifanikiwa, basi Samatta atapata nafasi ya kucheza katika hatua ya makundi Europa League.
Katika mchezo uliopita Samatta ambaye pia ni nahodha wa taifa Stars, alifunga bao katika sare hiyo iliyopatikana na wanakwenda katika mchezo huo wakiwa wametoka kushinda mchezo wao ligi ya Ubelgiji kwa mabao 3-0 Jumapili iliyopita huku Samatta akifunga mabao mawili kati ya hayo.
Kama Genk wakifanikiwa kupata sare ya bila mabao au ushindi mwembamba kuanzia 1-0 moja kwa moja watakuwa wametinga hatua inayofuata ya makundi ambayo ratiba yake inatarajiwa kupangwa Ijumaa
No comments:
Post a Comment