Most Popular

KLABU BINGWA BARANI ULAYA:MSN WAANZA KWA KUFUNGA MAGOLI ZAIDI YA TIMU NYINGINE YEYOTE ILE

Klabu bingwa Barani ulaya imanza tena.Mechi kali saba zilichezwa usiku wa kuamkia leo na kushuhudia mechi kati ya Man City na Borussia Monchengladbach ikiahirishwa kutokana na hali mbaya ha hewa...huku mechi nyingine zilichezwa kama ilivyopangwa.Yafuatayo ni matokeo ya Michezo hiyo:

FC Basel 1-1 Ludogorets

 

Kabla ya mapumziko,Jonathan Cafú aliiwezesha Ludogorets kuongoza kwa goli moja kwa bila
Lakini Basel walilipa kisasii mnamo dakika ya 80 kupitia kwa Renato Steffen na kufanya mechi kumalizika matokeo yakiwa 1-1

Man. City - Mönchengladbach: Imeahirishwa

Bayern Munich 5-0 FC Rostov:

 

Thomas Muller,Robert Lewandowsk na Juan Benart waliandika majina yao kwenye orodha ya wafungaji huku Joshua Kimmichi akifunga mara mbili kuwapa Bayern ushindi wa magoli 5-0 .

PSV Eindhoven 0-1 Atlético Madrid 

 

Saul Niguez alifunga katika kipindi cha kwanza goli lililoamua matokeo ya mchezo huo. 

Dynamo Kiev 1-2 Napoli:

 

 Kiev walifunga goli la kwanza kupitia kwa
Denys Garmash lakini Napoli walijibu kwa ufasaha kupitia kwa Arkadiusz Milk aliyefunga mara mbili na kufanya matokeo kumalizika 1-2

Paris Saint-Germain 1-1 Arsenal

Edinson Cavan alifungua mlango kwa Mabingwa wa Ufaransa mnamo dakika ya kwanza Lakini Alex Sanchez alihakikisha Arsenal wanaondoka na pointi moja mara baada ya kufunga goli la kusawazisha mnamo dakika ya 77.

Benfica 1-1 Besiktas:

Mnamo katika dakika ya 12, Franco Servi aliipatia Benfica goli la kuongoza,goli lilioonekana kuipa ushindi timu hiyo.Lakini Talisca alihakikisha Besiktas wanaondoka na pointi moja mara baada ya kufunga goli la kusawazisha mnamo dakika ya tatu ya mda wa ziada. 
Barcelona 7-0 Celtic 

Magoli matatu toka kwa Lionel Messi,Mawili toka kwa Luis Suarez,Moja likifungwa na Neymar la saba Likiwekwa kimiani  na Iniesta yalitosha kuipa Barcelona ushindi rahisi wa magoli 7 kwa bila dhidi ya Celtic.

hii inaamisha kuwa MSN wamefunga jumla ya magoli 6 katika ufunguzi wa mashindano hayo ,idadi ya magoli ambayo hayakuweza  kufungwa na timu yeyote ile katika ufunguzi wa mashindano hayo.

 



 
Posted By: MJOMBA ZECODER

KLABU BINGWA BARANI ULAYA:MSN WAANZA KWA KUFUNGA MAGOLI ZAIDI YA TIMU NYINGINE YEYOTE ILE

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger