Mshambuliaji nyota na nahodha wa
Uingereza Wayne Rooney anatarajia kustaafu soka la kimataifa baada ya
kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 itakayofanyika
nchini Urusi.
![]() |
Wayne Rooney kustaafu soka ya kimataifa baada ya kombe la dunia la mwaka 2018 |
Nyota huyo aliendelea kudai kuwa michuano hiyo itakuwa nafasi yake ya mwisho kufanya kila kitu na Uingereza hivyo bado ataendelea kufurahia miaka miwili iliyobakia.
Kama Rooney akicheza mchezo wa Jumapili hii wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Slovakia, atakuwa amevunja rekodi ya David Beckham ya kucheza mechi nyingi katika timu ya taifa.
No comments:
Post a Comment