Kinda wa klabu wa Manchester United, Marcus
Rashford, amefunga mabao matatu wakati akiichezea kwa mara ya kwanza
timu yake ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 21, wakati
walipoifunga Norway kwa magoli 6-1 kwenye mchezo wa kufuzu kombe la
mataifa Ulaya kwa vijana chini ya miaka 21.
Mshambuliaji
huyu kinda, tayari alishaifungia timu yake bao wakati alipoichezea kwa
mara ya kwanza kwenye mchezo wa Ligi kuu na Europa League sambamba ile
timu ya taifa ya wakubwa na sasa hii ya vijana walio na umri wa chini ya
miaka 21.
,
Rashford mwenye umri wa miaka 18 hivi sasa, aliifungia timu yake bao katika dakika ya 18 ya mchezo, akipiga shuti akiwa nje ya eneo la 18, kabla ya kuongeza bao akitumia mpira uliokufa na kisha kutamatisha kwa kuifungia bao la tatu timu yake kwa mkwaju wa Penalty.
Wachezaji wengine waliofingia timu yao ni pamoja na Nathaniel Chalobah, Ruben Loftus-Cheek na Lewis Baker.
Ushindi huu unamaanisha kuwa, kikosi cha kocha Gareth Southgate sasa kipo mbele kwa alama mbili dhidi ya Uswisi na kuongoza kundi lake, huku zikisalia mechi mbili tu.
Norway inasilia kwenye nafasi ya tatu kwenye kundi lake.
Timu zote zinazoongoza kundi, zinajihakikishia nafasi ya kucheza michuano hiyo mwakani nchini Poland huku timu inayomaliza kwenye nafasi ya pili katika kila kundi ikitakiwa kucheza mchezo wa ziada kufuzu.

No comments:
Post a Comment