Most Popular

Super Cup

BARCELONA YASHINDA 2-0 DHIDI YA SEVILLA ILIYOCHOKA

Mchezajı wa Barcelona,Lionel Messi akishika kichwa wakati wa mchezo wa kwanza wa Spanish Super Cup kati ya timu yake na Sevilla tarehe 14.08 .2016 kwenye uwanja wa Ramon Sanchez-Pizjuan,Sevilla.

Luis Suarez na Munir El Haddadi walifunga katika kipindi cha pili na kuipa Barcelona ushindi wa mabao mawili kwa nunge dhidi ya Seviila katika mchezo wa kwanza wa Super Cup nchini Hispania.
Katika dakika ya 54,Arda Turan kwa kutumia kifua Alimtengea mpira Luis Suarez ambaye bila kufanya kosa alifunga goli na kuiweka timu yake mbele kwa goli moja.Turan alipokea mpira huo toka kwa Dennis Suares
"Kipindi cha pili tulicheza vizuri zaidi" Alisema Luis Suarez."Turan ana mbinu nyingi mno,na alionesha hilo kwenye goli la kwanza" alimalizia kusema Luis Suarez.
Kunako dakika ya 81,Munil El Haddad aliihakikishia Barcelona ushindi kwa kufunga goli baada ya kupokea pasi toka kwa Lionel Messi
Katika mchezo huo,Barcelona iliwapoteza Andres Iniesta na Jeremy Mathiew baada ya wachezaji hao kuumia.Kabla hajaumia na kutoka,Iniesta alimpita mchezaji wa zamani wa timu hiyo,Carles Puyol kwa kuwa mchezaji wa pili wa Barcelona aliyeichezea timu hiyo mechi nyingi zaidi.Iniesta ameichezea Barcelona mechi 594.Nafasi ya kwanza inashikiliwa na Xavi Harnandez aliyeichezea Barcelona jumla ya mechi 767.
Kuumia kwa Iniesta na Mathiew kuliwapatia nafasi wachezaji Dennis Suarez na Lucas Digne kuichezea Barca mechi za za kwanza mara baada ya kusajiliwa na timu hiyo hivi karibuni
Sevilla,ambao walipoteza UEFA Super Cup kwa kuchapwa magoli 3-2 na Real Madrid,walionekana kuchoka dhidi ya Barcelona iliyokuwa ikicheza mechi yake ya kwanza ya msimu.
Kipa wa Sevilla,Sergio Rico alimzuia messi asifunge mara mbili baada ya Suarez kufunga goli la kwanza.
"Tulichoka katika kipindi cha pili sababu tulitoka kucheza na Real Madrid katika finali nyingine",Alisema Rico.
Spanish Super Cup huzikutanisha timu zilizoshinda La Liga na Copa del Rey.Lakini kwa kuwa Barcelona inashikilia mataji yote,Sevila ilialikwa kama timu iliyocheza finali ya kombe la Copa del Rey msimu uliopita.


Posted By: MJOMBA ZECODER

Super Cup

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© WWH-WORLD WIDE HABARI All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger