Mshambuliaji wa Manchester City
Sergio Aguero atakosa mechi ya debi kati ya timu yake na Manchester
United mnamo tarehe 10, Septemba baada ya kupigwa marufuku kwa mechi
tatu.
Aguero anayeichezea Argentina pia hatoshiriki katika mechi za Manchester City dhidi ya Bournemouth mnamo tarehe 17 Septemba pamoja na ile ya kombe la raundi ya tatu la EFL dhidi ya Swansea mnamo tarehe 21 mwezi Septemba
Aguero amefunga mabao matatu katika mechi tatu msimu huu na City ambao wako juu ya jedwali kwa kushinda mecho zote walizocheza.
No comments:
Post a Comment