Kiongozi wa chama cha upinzani
nchini Gabon, Jean Ping, amekata rufaa kwenye mahakama ya katiba
kupinga matokeo ambapo amesema aliibiwa kura kwenye uchaguzi wa mwezi
uliopita. Rais aliyekuwa madarakani Ali Bongo alishinda kuendelea
kuongoza nchi hiyo kwa kura chini ya elfu sita.
Bwana Ping amesema watu kadhaa wameuawa kwenye vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi , lakini serikali imesema kuwa ni watatu pekee ndiyo waliuawa.
No comments:
Post a Comment