Muungano wa vyama vya upinzani nchini Tanzania umeahirisha maandamano ya kitaifa ambayo yalikuwa yamepangiwa kufanyika LEO.
![]() |
Viongozi wa upinzani wakati wa kikao na wanahabari Dar es Salaam |
Viongozi wa chama hicho walikuwa wameitisha maandamano na mikutano ya kisiasa Septemba Mosi kupinga walichosema kuwa ni ukandamizaji unaoendelezwa na serikali.
Baada ya mkutano wa kikao cha Kamati Kuu ya chama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mwishoni mwa Julai, viongozi walisema: "Yapo Matukio ambayo yamekua yakifanywa na kukandamiza demokrasia na misingi ikipuuzwa na kudharauliwa."
Si nia ya Chadema kugombana na Serikali bali ni kazi ya Chama Pinzani kuisaidia Serikali iongoze kwa kufuata misingi ya Katiba," chama hicho kilisema.
Maandamano hayo yalipewa jina Ukuta, ikisimamia Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania.
![]() |
Bw Lowassa, ambaye aliwania urais kupitia Chadema katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka 2015 |
No comments:
Post a Comment