Korea Kaskazini inadaiwa kutekeleza 
jaribio la tano na kubwa zaidi la kifaa cha nyuklia, maafisa wa jeshi la
 Korea Kusini wamesema.
![]()  | 
| Maafisa wa Japan wanasema mitetemeko ya ardhi isiyo ya kawaida ilisikika | 
Maafisa wa Seoul wanasema mitambo yao iligundua tetemeko la ardhi ya nguvu ya 5.3 kwenye vipimo vya Richter karibu na eneo ambalo Pyongyang hutumia kufanya majaribio ya vifaa vya nyuklia.
Korea Kaskazini kufikia sasa haijasema lolote kuhusu jaribio hilo, lakini wachanganuzi wanasema hii huenda ikawa ishara ya hatua zilizopigwa na taifa hilo katika kustawisha teknolojia yake ya nyuklia.
Mitetemeko ya ardhi ya kusababishwa na binadamu ambayo imetokea eneo hilo awali yote ilitokana na majaribio ya nyuklia.
Bi Park, ambaye amesitisha ghafla ziara yake ng'ambo, amesema baada ya kutekeleza jaribio hilo la tano la nyuklia "serikali ya Kim Jong-un itakaribisha vikwazo zaidi na kutengwa zaidi na jamii ya kimataifa."
![]()  | 
| Eneo la Punggye-ri | 
Kupitia taarifa iliyotumwa na shirika la habari la Korea Kusini Yonhap, mkuu wa majeshi ya Korea amesema: "Tunakadiria kwamba Kaskazini imetekeleza jaribio kubwa zaidi."
Jaribio hilo linadaiwa kuzalisha nguvu ya kilotani 10, nguvu mara dufu ya jaribio lililotekelezwa Januari.
Wakati huo, Korea Kaskazini ilisema ilikuwa imtekeleza jaribio la bomu la haidrojeni.
Maafisa wa jiolojia wa Marekani, ambao hufuatilia shughuli chini ya ardhi, walisema awali kwamba mitetemeko ilisikika karibu na eneo la Korea Kaskazini la kufanyia majaribio ya nyuklia la Punggye-ri.
Ijumaa huwa ni Siku ya Taifa nchini Korea Kaskazini ambapo taifa hilo huadhimisha kuanzishwa kwa taifa la sasa.
Korea Kaskazini mara kwa mara hutumia majaribio hayo kuonyesha nguvu zake.
Japan imeshutumu jaribio hilo na Waziri Mkuu Shinzo Abe amesema inashirikiana kwa karibu na washirika wake.
Marekani pia imesema inafuatilia taarifa hizo.



No comments:
Post a Comment